habari yako mkuu, CAMI ni moja ya magari magumu sana ingawa watu wengi hawapendi show yake! kifupi vipuri havina shida vipo vingi sana! na gharama zake ni za kawaida
Spare za CAMI zinaingiliana na TERRIOS kwa hiyo inaongeza faida moja ya Cami. Gari hizi ni nzuri sana, zipo juu kiasi kwamba unaweza tumia mazingira yoyote mjini hata vijijini!
Tatizo kubwa watu wanaogopa CAMI ni gear box, but nikwambie kama unafanya service kwa wakati, hutopata tatizo hili hata siku moja!