Toyota Carina na biashara ya Tax nini mahusiano yake?

Toyota Carina na biashara ya Tax nini mahusiano yake?

The golden

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2018
Posts
1,382
Reaction score
2,582
Ukipita kwenye miji mingi hapa Tànzania katika Tax kumi utakazoziona basi angalau 6 zitakuwa ni Toyota Carina.

Je, gari hizi zimetengenezwa maalumu kwa ajili ya biashara hii? Imefika sehemu hata jina la gari zote zinazofanana kimuundo na Toyota Carina zikaanza kuitwa Tax.
 
Carina ina roho ya paka, spare parts bei ndogo na inaingiliana na matoyota mengi tu, hafu watoto wa mjini wanasema inanusa wese na AC kama Mufindi.

kuna mzee niliona ina ODO inasoma Laki 3 na ushehe.

Ila bodi bado inadai ndani safi na haigongi.
 
Ni gari imara kwa namna nilivyosikia, ni kama probox nazo zinasifiwa kwa ubora kulingana na barabara zetu.
 
Ukipita kwenye miji mingi hapa Tànzania katika Tax kumi utakazoziona basi angalau 6 zitakuwa ni Toyota Carina.

Je, gari hizi zimetengenezwa maalumu kwa ajili ya biashara hii? Imefika sehemu hata jina la gari zote zinazofanana kimuundo na Toyota Carina zikaanza kuitwa Tax.
Robustness ya Carina Ti ndio inafanya ziwe zinapendelewa. Zina matumizi mazuri ya mafuta, CC 1500. Pia spea zinapatikana kirahisi sana na kwa bei nafuu.
 
engnine ya 5A ni engene ngum sana unaweza itembelea hata km 30k bila kufanyia service na isizngue.

body yake ni pure metal body ngum mno na kitu kingine huwa hazichoki haraka ndani mafuta kidogo unatembea umbali mrefu
 
Sasa naanza kuelewa, kwa nini kila dreva Tax anaendesha Carina.
 
Kwanini hazitumiki kwenye uber/bolt?
 
Back
Top Bottom