Toyota Fortuner "Mjapan mwenye vinasaba vya Marekani"

denniehanda

Member
Joined
Apr 11, 2019
Posts
12
Reaction score
28
Kutoka hapa nilipo mpaka Ban-pho katikati mwa nchi ya Thailand ni kilometa 7191, Mbali kwelikweli.

Inaitwa Toyota Fortuner mid-size SUV mpango kazi wa kimarekani uliotekelezwa na Wajapan katikati ya viunga vya Ban-pho Thailand.

Akili inantuma kuamini kuwa Wajapani walitumia Mayakuza kuiba mbinu madhubuti za Mmarekani.Ukikutana na majasusi wa CIA huenda wakawa na siri niliyonayo mimi. Wapima vinasaba vya magari wanaweza wakawa na file lenye ukweli wa wapi ni asili ya Fortuner.

Ni bahati kufananishwa na Jeep Renegade, inatokea mara chache sana kufananishwa na Chevrolet Blazer. Awakukosea kuliita Fortuner wakimaanisha kitu chenye bahati.

Tegemea kukutana na Silver accents with wood like finish ukifungua macho yako mbele ya Fortuner. Hamna haja ya kuhubiri uwezo wa Fortuner. Ila andaa lita 80 za mafuta kujaza full tank gari hili.

Mimi bado naliita "The Godfather of the Road" ina nguruma kama simba mzee ikiwa Kwenye rami, ina engine ya diesel madhubuti CC 2982 na turbocharge kama ofa, kwanini iteseke sasa . Haitetemeki wala kuyumba hata ikiwa Kwenye speed ya 130Kmh. Ina sifa za kiasili za Kimarekani.

Kimo cha mjapan wa wastani ni futi 5 tu. Wao na Fortuner wapi na wapi[emoji3]. Maajabu ya Fortuner yanaelezwa mpaka Manhattan Newyork, Sitaki kukusimulia sana, maelezo utapewa pale Lumumba mtaa wenye madalali wakongwe, andaa peni na karatasi tu.

BRAVO! Toyota Fortuner Nabii wa Kijapan Aliyekubarika Dunia nzima. Ila bado najiuliza Fortuner kwenu ni wapi?[emoji848]

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Mkuu hapo kwenye R na L imekuaje tena?
 
Ila Jeep Grand Cherokee SRT za kuanzia 2014 zimesimama hatari...unakua na mnyama kama huo pembeni na mtoto mkareeeee....bongo kama mamtoni vile
 

Attachments

  • 8b38337135be7abb7923c26b82e59529.jpg
    29 KB · Views: 43
  • 68b5c54d3bbe7f7fab3658c44b37dff6.jpg
    60.8 KB · Views: 42
  • 99908624e5ec31efc28eb8305df8bc3d.jpg
    36.7 KB · Views: 39
  • 35f13e82e4e6393f2a2af019b9ceb0a3.jpg
    65 KB · Views: 38
  • 954877147f03aeac72c89990eca9bcf5.jpg
    14.5 KB · Views: 37
  • 4bea2d71539bf9b57e888df302f9b23a.jpg
    59.1 KB · Views: 34
  • 33acdbec520f6de7274e8f84fe75eaf6.jpg
    58.9 KB · Views: 33
  • c6ced874e1e93278c8b9855322f7e72a.jpg
    37.5 KB · Views: 37
Nmesikitika sana. Sijafahamu mleta mada ana tatizo gani.lakini nimeanza kuona pengine corona inaanza athiri hata fikra za watu.nme i google hiyo toyota aliyofananisha na magari.nikaelewa. kwa uelewa wake mwache aseme hivyo. Ila nmejisikia vibaya sana.anawezaje sema maneno hayo na sisi wengine tumo humu tunamsikia....ina maana anatuchukuliaje sisi?siyo sawa.hii ni thread ya kuudhi sana.

mkuu Kiduku Lilo unamaoni gani juu ya hii gari...!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…