Toyota IST na Toyota ALLEX ipi bora

Allex ni hatchback version ya Corolla. Corolla zipo models nyingi zikiwemo Spacio, Rumion, sedan yenyewe, Runx, etc. Kwa hizo gari kama ni za 1500cc utakuta zina share injini moja ambayo ni 1NZ-FE. Kwa ushauri wa manunuzi online, jifunze kutembelea mitandao ya wauza magari kama Beforward, SBT, nk. Pia website ya TRA kwenye calculator kujua ushuru wa gari husika. Tafuta angalau 13mil kupata moja kati ya hayo magari.

Samahani kwa kuvamia uzi, swali ulilielekeza kwa mtu mwingine.
 
Allion imesimama zaidi japo mi sio mpenzi wa Sedan, im more into Hatchbacks kama hio Alex/Runx.

Kwa 10m unapata Allion nzuri tu kibongo bongo, tena ukitaka kuna jamaa yangu anayo yake anaiuza bei hio hio. Ni mtunzaji mzuri wa gari, iko na Sport rims, Clean interiors plate ni DHF!
 
Allion ipo fresh zaidi ina more space lipo stable kwa barabara na ukizingatia service mzee utakaa nalo adi ulichoke,kuna jiran yetu flan apa wanalo wao kazi ni kuweka wese tu..mwaka wa 7 huu ipo fresh wala haijawah leta shida mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na pia kama unanunua kwa mtu angalia sana service plan yake ipoje na alikua na matumizi gani nalo usije ingia cha kike..kuagiza ni vizuri japo inabidi uongeze kidogo apo walau 14m ivi kwa hapo uhakika unapata kitu maini kabisa as of odometer 22,000km au below

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…