Satoh Hirosh
JF-Expert Member
- Mar 30, 2021
- 6,432
- 25,646
Habari wakuu,
Kuna huyu mdogo wetu kitaani hapa amemaliza chuo miaka kadhaa iliyopita ila yupo home Hana mishe za kueleweka. Sasa Mzee kastaafu na ameshachukua kiinua mgongo. Dogo amemwomba Mzee anunue gari ili awe anapiga mishe za taxi mtandao(Uber,bolt nk).
Chaguo lake yeye lilikuwa ni Toyota IST,lakini Mimi nikamshauri achukue toyota Aqua maana ni hybrid car Ina ulaji mzuri wa mafuta inaenda hadi 30km/h hivyo kwa Biashara ya taxi itakuwa nzuri kuliko IST.
Hilo lilikuwa pendekezo langu Mimi.
Ila yeye akaja na hoja kadhaa ambazo ni kama amenichallenji nimeshindwa kutetea hoja yangu.
Hoja zake anasema;
1.Aqua imekaa kimayai haiwezi kuhimili shida na routes za off-road kulinganisha na IST. IST anazikalisha gari nyingi mdogo kwenye hili ikiwemo na hii gari yangu niliyoipendekeza. Anasema IST gari ngumu haiwahi kuchakaa hasa ukizingatia itakuwa inapiga kazi karibia Kila siku,hivyo akaikataa gari Aqua katika hili.
2. Ground clearance.
Anasema Aqua ipo chini sana kulinganisha na IST,hivyo anaiona ni gari ya kwenye lami pekee. Akaniuliza vipi nikipata wateja wa bonyokwa na maji matitu niwakatae?
Kwa kifupi dogo ameikataa kabisa aqua na kung’ang’ania IST ingawa kwa hoja zake bado Mimi nilikuwa napendekeza aqua maana ni latest kuliko hiyo IST ya 2001.
Nimeona niletee humu ili kupata maoni tofauti kutoka kwa wajuzi na wataalamu wa magari,maana Mimi siyo mjuzi wa hilo eneo,japo nimempa ushauri dogo.