Toyota Mark X nataka kujuwa zaidi kwa wale wengine wanazozitumia kama kuna common changamoto wanazokutana nazo zaidi ya kujaza full tank Ltrs 70 na uchumi wa sasa. Kwenye kuitumia kwa matumizi ya kila siku nini kinajitokezaga mbeleni. Juzi tuu nilienda kwa fundi wangu nayemuamini akaniambia hii kitu ikikwama porini usiniite, nikuvuta tuu mANake parts zimefichwa sana kwenye engine mpaka kukifikia kama ni kitu kikizingua na jinsi ilivyo chini.
Juwa matumizi ya PWR.
Hizi mvua mvua juzi Kati hapa ziliniweka mahali kama karibia Lisaa hivi tairi zilikuwa zinazunguka tuu gari haitaki kwenda. Lakini mwishowe nikabonyeza kile kitufe cha PWR ECT aisee gari ilienda yenyewe kama ilikuwa imeingizwa fwd hivi. Kumbe hii pwr kwenye njia zetu hizi za tope kinasaidia.
Matatizo ya engine kusumbua mara nyingi ni matunzo hapa ni kilainishi oil au fundi amekuaribia kwa kushindwa kuelewa ugonjwa kwa wakati. Mafundi wetu wengi wataalamu kwenye magari ya zamani haya yenye umeme mwingi lazima usimamie ukiona kitu hakielewi muambie aache utafute anayeweza.
Hii ilikuwa na tatizo lita 70 ukupe 220km ni kama ilikuwa inavuja. Miye nikifanya Fujo kimjini hapa na mafoleni angalau km 400 naisogeza. Masafa marefu mpaka 500km ila ninaongezeaga inaweza enda zaidi