Toyota Spacio 4WD (Four Wheel Drive )

mdoghosho

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2016
Posts
969
Reaction score
1,383
Wakuu, Naomba kujua kuhusu UIMARA na ULAJI MAFUTA wa Spacio yenye cc 1790 ambayo ni Four Wheel Drive.

Naomba kujua Ubora na Udhaifu wake ukilinganisha na ile Spacio yenye cc 1490 ambayo ni 2WD

Ninahitaji hii Gari kwa Matumizi ya Milimani huko kijijini kwetu Upareni.

Nisaidieni mawazo wakuu, Nahitaji kuagiza gari Japan week hii.
 
Hilo gari hata kwa macho tu linaonekana body lake ni laini ..sehemu mbaya mbaya litawahi kuchoka
 
Hivi Hamna mwenye experience ya hili gari humu?
 
Uzuri
Ni jamii ya corolla spea bwerere
Injini vvti so inakula wese kidogo
Kuna zenye siti 7 so unaweza pakia watu wazima 5 na vitoto 2!!
Ubaya
Iko chini ingawa waweza eka spacer na tyre ya profile kuibwa ikainuka kidogo
Hizo siti mbili za mwisho ni ndogo so wakikaa watu wazima watajibana
4wd yake ni full time
Si nzuri saana kwa shoruba maana sio suv

Agiza tu mkuu maana kwa kwa cc hizo ni toyota chache sana zenye 4wd.hata bei ya kuagiza ni ya kawaida sana ila nikupe angalizo nunua kutoka kwa muuzaji ambaye ni reliable na upate kampuni nzuri ambao watafanya ukaguzi kabla halijatumwa bongo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…