Toyota Vs Nissan

Lokii

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2016
Posts
709
Reaction score
2,089
Habarini wanaJF

Katika pitapita zangu hapa mjini nimekuwa nikiona magari mengi watu wanayomiki ni toyota hata nikiwa ndani ya daladala kwenye foleni huwa naona magari mengi kwenye foleni ni toyota yani katika magari kumi utakuta sita ni toyota labda mawili ni nissan na mengineyo

Kiujumla naweza kusema magari ya toyota ni mengi zaidi hapa mjini kulinganisha na nissan Sasa nataka niagize gari langu la kwanza la nissan la kutembelea lakini nimekuwa nikijiuliza kwanini magari ya nissan sio mengi kama toyota?
Kwanini watu wengi wanapendelea zaidi magari ya toyota? Kulikoni?

Kuna wadau niliwauliza wakasema ni kwasababu spea za gari za nissan ni ghali kuliko toyota
Napenda kupata uzoefu wenu wakuu baina ya magari ya toyota na nissan hasa kwa wale ambao wameshamiliki magari aina zote hizi mbili

Angle of view;
-› Uimara(durability) ya magari ya toyota vs nissan
-› Urahisi wa kupata vipuri/spea
-› Mafundi wazuri waliopo

Nawakilisha...
 
Ni vyema mkawa mnapenda kusoma vya wenzenu sio ubinafsi uliowajaa kutaka watu wasome vyenu na msaidiwe. Humu kuna nyuzi kibao zimeshazungumzia tofauti ya makampuni hayo mawili ya magari.
 
Ni vyema mkawa mnapenda kusoma vya wenzenu sio ubinafsi uliowajaa kutaka watu wasome vyenu na msaidiwe. Humu kuna nyuzi kibao zimeshazungumzia tofauti ya makampuni hayo mawili ya magari.
Mkuu JF ni kama pori ujue, sio kila uzi wa zamani ntaweza kuuona na ukizingatia mi mgeni hapa JF ingawa nimekuwa msomaji mzuri tu nikiwa nje kabla sijaamua kujiregister hivi majuzi... Anyways turudi kwenye mada baadhi ya nyuzi nlizozipitia zinazofanana na hii nyingi utaona zilizungumzia tofauti ya gari flani flani specific baina ya toyota ama nissan, mi ukiangalia uzi wangu sijaspecify upande wa toyota ama nissan
Nilitaka tu kujua(kwa magari ya kawaida tu ya kutembelea) ni kwanini watu wengi wana-prefer toyota??
 
nissan huwezi fananisha na toyota mkuu.nissan ni gari zuri sana na siku zote kizuri garama.spea zake ni grama lkn sio kwa kiwango cha wauzaji wetu wakibongo.mm nakushauri kamata nissan tuu
 
Lege ni kweli Nissani ni gari zuri ila umeongelea kwa ujumla wake maana yapo Toyota mazuri na hovyo pia na vivyo hivyo Nissani zipo nzuri na za hovyo pia kwa hiyo mjadili kutokana na model ya gari...kwa hiyo hata Toyota hard top ni za hovyo kwa maelezo yako mkuu..
 
nissan huwezi fananisha na toyota mkuu.nissan ni gari zuri sana na siku zote kizuri garama.spea zake ni grama lkn sio kwa kiwango cha wauzaji wetu wakibongo.mm nakushauri kamata nissan tuu
Asante kwa ushauri mkuu, vipi hizo spea za nissan ni mpaka uagize au zinapatikana tu hapahapa?
 
kama hauna hela ya kutosha usipende kununua magari ambayo mtaani yapo machache. kuna Mitsubish moja ipo ilikuwa inasumbua sana tukaambiwa tatizo ni plug, tunaenda kununua plug dukani moja ni shilingi elfu ishirini na tano, sasa zinahitajika nne hapo ni laki, sasa hela ipi lakini plug original hazipo ukizipata unapata plug feki mwezi zimezingua, ukitaka original ni mpaka upate za mitumba/used na huo ni mchakato hapo option ni kuagiza nje, limesumbua option ya mwisho tukaona bora ibadilishwe engine tu.
 
Mkuu spea za nissan zipo tele..maduka yapo mengi kwa dar ni mastercard..kisangani etc along msimbazi road.
Hapo mastercard pasikie tu, wao ndio wanafanya watu waziogope nissan, nilienda kununua kifaa jamaa akaniambia laki 270 na kodi kaishapiga hapo hapo.. Nikajidai nakuja ngoja nmalzie vingne, kwenda maduka ya mbele kifaa kile kile 70 elf na risit ya kodi nikapewa imekatwa kabisa ktk hyo 70 elfu..
 
Bob Nissan ni gari nzuri lakini inahitaji matunzo.... Na kuhusu spare Nissan nyingi HAZINA spare za kuchakachua ndio maana Bei yake iko juu.... Pia sio mafundi wote wanajua kutengeneza nissan , Toyota zinapendwa sababu spare zinapatikana...... Na Bei ni rahis sababu nyinhine ni za kichina

Samsung J7
 
Binfasi nimeshamiliki Toyota Hilux na sasa namiliki Nissan Navara 2.5 Di zote manual nilichogundua Nissan ina nguvu sana kuliko Toyota kwa hizi SUV ukiiendekeza inaweza kukusababishia majanga lakini pia Nissan ukiweka spare fake haikubali yaani baada ya siku mbili tatu tatizo linarudi pale pale hadi uweke genuine tofauti na toyota.
Angalizo;Sina maana Toyota ni gari mbaya lakini kwa uzoefu wangu Nissan ipo juu ya toyota kwa perfomance
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…