mwengeso
JF-Expert Member
- Nov 27, 2014
- 9,227
- 6,670
Waziri wa Fedha akijibu swali "kwa nini anayetuma na anayepokea fedha wote wanatozwa?" Jibu lake limeacha swali lingine.
Hakika anayepokea anapaswa kutozwa kwa kuwa anapata kipato. Anayetuma tayari atakuwa ametozwa pale alipopata hiyo fedha hivyo hastahili kutozwa tena.
Kwa mfano alioutoa wa fundi wa nyumba ambaye amelipwa kwa mwamala akatozwa, endapo atanunua vifaa vya ujenzi kwa mwamala atatozwa mara ya pili, na aliyelipwa naye akifanya mwamala mwingine atatozwa tena. Kwa mtiririko huo fedha hiyo itakuwa imepungua thamani yake.
Mfano tozo la Serikali kutuma 10,000/- ni 2,120/- (1,800/- gharama za mtandao + ni 320/- tozo ya Serikali), jumla anayetuma ni 12,120/-. Aliyepokea akiamua kutoa kwa wakala atatozwa tozo la Serikali 320/- tena na gharama za mtandao 1,800/-, salio ni 7,880. Akiamua kumrushia mtu mwingine atatozwa kiasi hicho hicho (2,120/-) na mpokeaji atapokea 5,760/-. Huyu akiamua kutoa kwa wakala atatozwa gharama za mtandao na tozo la Serikali. Thamani ya fedha ya awali (10,000/-) ni kama hakuna.
USHAURI: Gharama za kutuma fedha kwa mitandao zipunguzwe na tozo ya Serikali iondolewe ili kulinda thamani ya fedha na kuongeza mzunguko wake katika miamala