Tozo na kodi za kizalendo ziende kwenye matumizi na miradi ya Kizalendo

Tozo na kodi za kizalendo ziende kwenye matumizi na miradi ya Kizalendo

Gift mzalendo

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2019
Posts
1,856
Reaction score
2,417
Heshima kwenu wakuu

Kwanza nikiri sisi Kama taifa tunawajibu wa kulipa Kodi kwa ajili ya kujenga taifa letu.

Pili, Hakuna mtanzania Mzalendo ambae hapendi kulipa Kodi au Kodi kwa ajili ya ujenzi wa nchi yake

Tatu, Bila Shaka yoyote Kila mtanzania amehusika kujenga nchi hii kwa kulipa Kodi moja kwa moja au kwa namna moja au nyingine.

Hapa nisisitize kiuhalisia hakuna matajiri au makampuni yanayolipa Kodi, isipokuwa wananchi (walaji wa mwisho) wanaonunua hizo bidhaa na huduma za makampuni, ndo wanalipia gharama na kodi za bidhaa au huduma husika.

Kwanini Sasa wananchi tunapingana na tozo na Kodi mpya Kama zilizopitishwa juzi ?

Moja, Hakuna ushirikishwaji wa malengo ya pamoja Kama taifa, haiwezakani Kila mtu aje mipango yake bila kushirikisha kikamilifu wanaolipia gharama za hiyo miradi

Pili, matumizi yake hayana malengo maalum (specific) na Kama yapo raia hawana uelewa wa kutosha namna taifa litanufaika na hiyo miradi

Tatu , Wananchi kupunguza imani kwa serikali juu ya usimamizi na nidhamu ya matumizi ya Kodi na tozo zake, kwa sababu usimamizi mbovu na kukosekana kwa nidhamu ya matumizi inaweza kuvunja moyo walipa kodi

Nne, Serikali kumilikisha Kodi kwa mtu mmoja au kikundi Cha watu, hivyo wananchi kuona kwamba hawana mchango wa moja kwa moja kwenye maendeleo yao, hii haivunji moyo tu watanzania walipa Kodi, inaondoa team work kwa watumishi wa umma na mfumo wa serikali,Kwa Wenzetu wanatumia kodi kwa hisani ya watu wa Marekani ,nk

Tano, kukosekana kwa miradi yenye vipaumbele vinavyogusa wananchi moja kwa moja,
Tunajua Kuna miradi ya muda mrefu na ya muda mfupi, miradi mingi Ilenge kuboresha mazingira ya ukuaji wa uchumi kwa walipa Kodi.

Kama maendeleo ni ya wanachi,

Ushirikishwaji wa wananchi ni muhimu sana katika mipango matumizi na ukusanyaji Wake
 
Back
Top Bottom