Tozo ya miamala, Ugaidi wa Mbowe na Ujio wa Chanjo ya Corona

Tozo ya miamala, Ugaidi wa Mbowe na Ujio wa Chanjo ya Corona

Recipient

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2014
Posts
425
Reaction score
345
Wanabodi,

Kama watanzania tunapitia katika changamoto nyingi lakini kubwa tatu.

Wakati bado serikali halijapatia ufumbuzi malalamiko kuhusu Tozo ya Miamala ambayo bado imekuwa kero kwa wananchi, likaibuka suala la kukamatwa Mbowe anayetuhumiwa kwa makosa ya kupanga ugaidi.

Wakati hili la Mbowe bado halijapoa likaja taarifa za serikali kupokea chanjo ya Johnson and Johnson iliyowasilishwa nchini na kampuni ya usambazaji ya Covax.

Ukweli Tanzania tunapitia kipindi kigumu, kwanza Tozo, pili taarifa ya maambukizi ya corona yaliyoibuka ghafla baada ya kifo cha baba yetu Magufuli, tatu kukamatwa kwa Mbowe, na nne mapokezi ya chanjo ya Johnson and Johnson.
 
Kuhusu swala la chanjo si lazima, una haki ya kukubali kuchanjwa au kutokubali, kikubwa ni kupata taarifa sahihi kutoka kwa wataalamu wa afya..

Kuhusu suala la Mh. Mbowe, mchakato mzima wa kumkamata na hata jinsi kesi unavyoendeshwa ni kinyume cha haki za kibinadamu na misingi ya sheria na katiba, ubabe na ukiritimba, na chuki zidi ya upinzani ndio umetawala....

Suala la tozo za miamala ya simu linadhihirisha kupwaya kwa serikali hasa katika kukusanya taarifa ambazo zinasaidia katika kufanya maamuzi, walakini wa taaluma za viongozi wafanya maamuzi na umakini wa muhimili wa Bunge
 
Nchi haina kiongozi hii tunajiendea tu kama wakati ule wa Msoga, hawa jamaa wanashindwa kabisa kuficha udhaifu wao kiuongozi.
 
Mbowe anakabilwa na mashitaka mazito na hatari sana ya ugaidi, alipo kuwa anaweka mipango mikakati hatukuwepo hivyo wacha apambane na hali yake.
 
Mbowe anakabilwa na mashitaka mazito na hatari sana ya ugaidi, alipo kuwa anaweka mipango mikakati hatukuwepo hivyo wacha apambane na hali yake.
Tangu aliposema account zake zimefungwa na TRA kumbe ni kutokana na kesi ya kifamilia simuamini Tena mwenyekiti wa kudumu.
 
Wakati bado serikali halijapatia ufumbuzi malalamiko kuhusu Tozo ya Miamala
Mama amesema tozo zitaendelea haipungui hata senti moja. Anataka fedha za kukamilishia miradi
 
Mama amesema tozo zitaendelea haipungui hata senti moja. Anataka fedha za kukamilishia miradi
Unamlisha maneno, tozo kwa maana za miamala zitanedelea ila wtaaboresha ili asiumie sana mwananchi kwa maana sheria ipo ila kanuni zitabadilishwa
 
Tangu aliposema account zake zimefungwa na TRA kumbe ni kutokana na kesi ya kifamilia simuamini Tena mwenyekiti wa kudumu.
Kuvunjwa kwa Club Billicanas, na green house zake Moshi was it a family matter? Chama Cha Mazezeta mna shida sana nyie
 
Back
Top Bottom