SoC01 Tozo ya miamala ya simu: Uwanja umeinama, Tuangazie Kilimo kitatukomboa

Stories of Change - 2021 Competition
Joined
Jul 16, 2021
Posts
25
Reaction score
25
Na ,Ibrahim Rojala

Kuanzia Julai 15 ya mwaka huu wanaotuma fedha kwa wakala wa simu za mikononi walianza kulipa kodi ya uzalendo ambayo waziri wa fedha Dkt.Mwigulu Nchemba aliielezea kuwa ni muhimu kulipwa.

Kupitia makato mapya ya miamala ya simu kiasi cha chini cha kodi ya uzalendo ni shilingi 10 makato ya juu kwa mtu anayetuma fedha yakiwa 10000 kiasi cha ongezeko la gharama za kutuma au kutoa fedha kwa wakala kutokana na kodi mpya kikiwa 1100%.

Wakati hali ya mambo ikiwa imebadilika kwa kiwango kikubwa namna hiyo kuna maswali mengi ambayo majibu yake yamebaki kuwa mashaka kwa walio wengi wanaoguswa moja kwa moja na takwa la kuoonesha uzalendo kupitia miamala ya fedha kupitia mitandao ya simu.

Swali la kwanza ni kutoka kwa mawakala 300000 waliopo nchini wanaotoa huduma za kifedha kupitia mitandao ya simu ambao wanajiuliza je kiwango cha wateja hakiwezi kupungua kutokana na makato ada za miamala kupanda kwa kiasi kikubwa?

Kabla ya kuangazia zaidi kuhusiana na makato napenda kutazama uzalendo ulioleta kodi hii

Uzalendo ni hali ya mtu kuipenda, kuithamini na kujitoa kwa ajili ya nchi yake.

Mzalendo wa kweli daima anaweka maslahi ya nchi mbele na ya kwake binafsi nyuma. Kwa maana hiyo hapo juu, mzalendo ni mtu yeyote mzawa na mwenye kuipenda na kujitoa mhanga na saa nyingine ikibidi kufa kwa ajili ya nchi yake.

Uzalendo unabeba dhana nyingi sana ikianzia asili, utamaduni, lugha, siasa, historia, nk. Dhana zote zikifungwa kwenye dhana kuu ya utaifa.

Baada ya kuelewa maana ya uzalendo turudi kwenye hoja ya msingi,uzalendo kupitia miamala ya simu,ajenda iliyoibuliwa na mbunge wa Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan Zungu akizungumza bungeni alipokuwa akichangia mjadala wa kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Rais (Tamisemi) kwa mwaka wa fedha 2021/2022 jijini Dodoma Aprili 20 ya mwaka huu.

Kodi hii imeongeza idadi ya kodi ambazo mwananchi alikuwa analipa kutoka mbili hadi tatu ambapo awali alikuwa akilipa ushuru wa forodha ambao ni asilimia mbili na kodi ya ongezeko la thamani (VAT) asilimia 18%,kodi ambazo tayari zilikuwepo zilikuwepo.

Kodi hii inakuja pia katika kipindi ambacho laini za simu zinapaswa kulipiwa kodi kama ilivyoelezwa katika Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Waziri wa fedha Mheshimiwa Mwigulu Nchemba alieleza kwamba laini hizo zitakuwa miongoni mwa vyanzo vya fedha zitakazotumika kutekeleza miradi ya Maendeleo,maelezo yaliyotolewa Juni 10 mwaka huu alipokuwa akiwasilisha bajeti kuu pendekezwa ya serikali kwa mwaka 2021/2022.

Haya yanajiri katika kipindi ambacho kumekuwa na kukua kwa kasi kwa sekta ya mawasiliano nchini ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa laini za simu za mkononi zilizosajiliwa kutoka 48,939,530 Julai mwaka 2020 hadi 53,063,085 Aprili 2021; sawa na ongezeko la asilimia 10.8.

Katika kipindi hicho pia akaunti za matumizi ya huduma za pesa kupitia simu za mkononi zimeongezeka kutoka 27,127,298 Julai mwaka 2020 mpaka 32,720,180 Aprili, 2021; sawa na ongezeko la asilimia 20.6.

Kwa mujibu wa mfumo wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania wa kusimamia na kuratibu mawasiliano ya simu (TTMS),jumla ya shilingi Shilingi 170,513,110,859,867 zilitumwa na kupokelewa kupitia huduma za pesa kwa njia ya simu za mkononi kati ya tarehe 1 Julai 2020 na 30 Aprili 2021.

Kwa takwimu hizi tunapata picha halisi kwa kiasi gani huduma hii imekuwa ni sehemu ya maisha ya watanzania na muhimu sana kwa ukuaji wa uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

Huduma hii imeokoa muda,kupunguza matukio ya unyang’anyi,kutoa ajira na hata kukuza biashara pamoja na kuwaunganisha watanzania hususani katika maeneo ambayo huduma za kibenki na posta hazijaweza kufika.

Binafsi nilitarajia uwepo wa mabadiliko ya tozo za miamala ya simu kwakuwa nilikuwa mfuatiliaji mzuri wa vikao vya Bunge la 12 la Bajeti,lakini sikutarajia kuwa mabadiliko hayo yangekuwa kwa viwango vikubwa kiasi cha kuzua hamaki kwa baadhi ya watumiaji wa huduma hii.

Ukiangalia mijadala mingi katika mitandao ya kijamii ni ile iliyojikita katika kutafuta mbinu mbadala za kuweza kutuma fedha katika hali ya kukwepa gharama za makato mapya huku wengine wakieleza kuwa kwa baadhi ya maeneo kutokana na umbali aliopo mtumaji na anayetumiwa ni bora kupeleka fedha kwa usafiri kuliko kutuma.

Kwa wapenda soka watakuwa wanaelewa ni kitu gani ninachomaanisha nikisema uwanja umeinama,ongezeko la tozo limekuja katika kipindi ambacho kumekuwa na baadhi ya bidhaa za vyakula zilizoongezeka bei kwa Mei, 2021 zikilinganishwa na bei za Mei, 2020 ambazo ni unga wa ngano kwa asilimia 4.1, nyama kwa asilimia 4.0, viazi mviringo kwa asilimia 7.5, mihogo mibichi kwa asilimia9.2, ndizi za kupika kwa asilimia 2.4, maharage kwa asilimia 5.0 na njegere kwa asilimia 7.1.

Uwanja umeinamia zaidi kwa wananchi wa kawaida ambao wengi miongoni mwao hawana akaunti za benki ambazo walio mijini wanaona ni bora wafanyie miamala yao huko.

Wakati hali ikiwa hivo kwenye miamala ya simu bado tunapaswa kukumbuka ongezeko la shilingi 100 kwenye kila lita ya mafuta fedha itakayotumika katika kuboresha miundombinu ya barabara.

Kodi hii ya miamala ya simu inatarajiwa kuiwezesha serikali kukusanya kiasi cha shilingi trilioni 1.2 lakini kwa malalamiko ninayoyaona na kuyashuhudia mitaani napatwa na shaka kama lengo linaweza kutimia.

Najiuliza kuwa je ni kuwa hatuna vyanzo vingine mbadala vya kukusanya mapato tofauti na hivi,kama ni mwananchi wa kawaida anapaswa kulipa kodi badala ya kuwategemea wafanyabiashara wakubwa 500 pekee walioelezwa kutegemewa kulipa kodi nchini je wananchi wa kipato cha chini hawalipi kodi?

Inatafakrisha,kama bunge lina jukumu la kuishauri serikali na kutunga sheria,nani analishauri bunge?maana huenda wawakilishi wetu hawajui hali halisi ya maisha yetu huku mtaani.

Huenda hawajui kuwa wazazi wetu walioko pembezoni hata wakikohoa kikohozi cha kawaida kitokanacho na umri kwenda na kinga ya mwili kupungua huitaji tuwatumie walau 5000 wakanunue dawa.

Kwa hali ya mambo ilivyo wazee wanaweza wakajua vijana tumewehuka huku mijini,wale wa tuma na ya kutolea inaweza kubaki historia lakini mbaya zaidi naliona anguko katika biashara kwa wale tuliozoea kulipana kwa njia ya miamala.

Ongezeko hili pia linakuja katika kipindi ambacho Ripoti ya hali ya Uchumi Tanzania toleo la Juni 2020 kutoka benki ya Dunia(WB) ilionesha kuwa ni asilimia 23.4 pekee ya Watanzania waliopo mijini wana akaunti za beki lhali asilimia 5.1 pekee ya watanzania walioko vijijini wanatumia akaunti za benki.

Aidha ripoti hiyo ilieleza kwamba namna pekee ya kuwajumuisha watanzania wengi katika huduma za kifedha ni kupitia huduma za kifedha za simu.Hii ni kuashiria kwamba ni huduma pekee ambayo inamgusa kwa kiasi kikubwa kila mtanzania kwani hadi kufikia mwezi April Mwaka huu kati ya watumiaji wa simu milioni 53,watu milioni 32 kati yao wanatumia huduma ya kifedha kwa njia ya mitandao ya simu za mkononi.

Uzalendo naamini watanzania wanao,ndio maana wanalinda na kuithamini tunu ya amani mpaka leo,naamini wanalipa kodi hata kupitia bidhaambalimbali wanazonunua,huduma nyinginezo wanazotumia na hata miamala ya fedha kama ilivyokuwa awali.

Kodi hii ambayo imekuja katika kipindi ambacho hatupaswi kufanya safari zisizo za lazima kutokana na uwepo wa Covid-19 itatufanya upigane vikumbo katika vyombo vya usafiri bila ya kuchukua tahadhari tukiwa na lengo la kupeleka fedha mahala tunakohitaji zifike.

Tunapaswa kulitafakari hili ili tusije kujikuta tunarudi nyuma katika ulimwengu wa Tehema badala ya kusonga mbele, msemo maarufu kwa sasa”usinambie nikutumie fedha kwa njia ya simu,ifuate au nitakuletea”maana uwanja umeinama.

Ni wakati wa kuangazia vyanzo vingine vya mapato kuliko kujikita zaidi katika kodi pekee,tuboreshe kilimo nchini ili kivutie watu wengi kujikita huko ili tuuze mazao nje na kuongeza pato la taifa,tusimamie rasilimali zetu mathalani madini,wanyamapori mazao ya maziwa bahari na mito yetu hatua mabayo itasaidia katika kutanua biasharaza kikanda,Afrika nzima na Dunia kwa ujumla kuliko wazo letu la kwanza kama taifa kuwa kodi,tukimkamua sana bila kumlisha vyema ipo siku badala ya kutoka maziwa itatoka damu.

Kama sekta nyingine zimekuwa ngumu kwa sisi wenyewe kama taifa kuzisimamia kutokana na kukosa mtaji wa kutosha mathalani kama sekta ya madini,basi ni vyema nguvu zote tukaziweka katika kilimo,sekta ambayo imeajiri watanzania wengi na inayoweza kuzalisha rasilimali nyingi ambazo zitalisha viwanda ambavyo serikali imekuwa ikisema kwmba ni Tanzania ya Viwanda.

Tunapaswa kwa uzito mkubwa na dhamira ya dhati tukiongozwa na uzalendo wa kweli kuibeba na kuifanyia kazi kauli ya mwenyekiti wa Bodi ya AGRA, Waziri Mkuu Mstaafu wa Ethiopia, Hailemariam Dessalegn, ambaye July 13 mwaka huu akiwa wilayani Bagamoyo mkoani Pwani alisema Tanzania inaweza kuilisha Afrika iwapo mapinduzi ya kilimo yatafanyika kwa umakini na kwa ukamilifu.

Si dhambi kurejea makabatini na kutafuta maandiko muhimu tuliyoyaandaa ili kutekeleza mpango wa matokeo makubwa sasa(BRN) na kuangalia namna ya kutekeleza mpango huo badala ya kutegemea kodi kuwa chanzo kikuu cha mapato kwa nchi.

Ninaamini katika matokeo makubwa sasa kupitia kilimo kwasababu ushahidi wa nyakati ambazo tuliwahi kufanikiwa upo, Tanzania chini ya BRN, ilishuhudia uzalishaji mkubwa wa mahindi na mpunga katika msimu wa 2013/14; jambo ambalo lilileta matumaini kwamba tunaweza kufikia malengo tuliyokusudia.

Ikiwa tupo katika nchi ambayo ina eneo la hekta milioni 44 ambaloni sawa na aasilimia 46% ya ardhi yote tuliyo nayo linalofaa kwa kilimo na eneo lililotumika mpaka sasa kwa shughuli za kilimo halijafika hata asilimia 30%basi ni vyema tukajikita katika kilimo kwasababu fursa ya soko ipo kutokana na hali ya mahitaji ya chakula duniani kwani kwa kipindi cha mwaka jana takribani watu milioni 811 duniani walikuwa hawana lishe bora.

Tutumie kilimo kama fursa ya kutuvusha,kodi nyingi hazitotufikisha tunapohitaji kufika kama taifa na zitazidi kuumiza wanyonge.
 
Upvote 16
Asante mkuu kwa andiko zuri. Lugha maridhawa na mpangilio mzuri.

Naunga mkono hoja ya kurejea kwenye makavazi yetu kufufua mipango yetu mizuri ya kuinua kilimo chetu.

Hata hivyo,ili tuwe na uchumi shirikishi ambao kila mwananchi anashiriki kujenga na ili kukuza utamaduni na moyo wa kulipa kodi,tozo za miamala ziendelee kama zilivyianzwa kutekelezwa.
 
Kubwa sana hi I
 
Andiko zuri
 
Andiko zuri broo, safi.
 
Asante mkuu kwa andiko zuri. Lugha maridhawa na mpangilio mzuri.

Naunga mkono hoja ya kurejea kwenye makavazi yetu kufufua mipango yetu mizuri ya kuinua kilimo chetu.

Hata hivyo,ili tuwe na uchumi shirikishi ambao kila mwananchi anashiriki kujenga na ili kukuza utamaduni na moyo wa kulipa kodi,tozo za miamala ziendelee kama zilivyianzwa kutekelezwa.
shukrani sana mazagazagatza.
 
well said bro umeongea ukweli mtupu
 
Kama ingekuwa siasa ningem quote mr II sugu kuwa u ni "uandishi wa Mars ". Out of this planet
 
tuletee nyingine nyingi kama hizi kaka tupate vitu kichwani tuweze kuwaza fikra chanya kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi

Kubwaa saanaaa hiii Shukrani kwa andiko Zuri
 
Back
Top Bottom