tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 24,225
- 22,632
Ndugu zangu naandika hii taarifa nikiwa mnyonge kama kinda la ndege lililonyeshewa na mvua ya mawe baada ya kutelekezwa na mama yake. Sitaki kuwachosha na maneno mengi ngoja niende kwenye mada moja kwa moja kwa kuwa wengi wetu tumechoshwa na tozo hizi za mchongo zinazotukamua na kutuacha bila kitu. Hii ni zaidi ya kumkamua ng’ombe kila kukicha bila kumlisha chakula chochote. Ipo siku ng’ombe huyu atakata roho na hapo ndipo mkamuaji atakapolia na kusaga meno kwa kumpoteza ng’ombe kwa ujuha wake mwenyewe.
Ndugu zangu, nchi hii imekuwa ngumu sana. Kwa wale tunaoweza kuhamia Burundi afadhali tuanze safari mapema kabla hali haijawa mbaya zaidi. Huu ukamuaji tunaokamuliwa hapa nchini sio wa kawaida hata kidogo. Kuna taarifa za chini chini kutoka kwa watu waliomo jikoni kuwa baada ya matokeo ya sensa kuweka hadharani hapo tarehe 31/10/2022, serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango, chini ya mchumi msomi Dr Mwigulu Madelu Nchemba (PhD & Hons) itaanza mara moja kutoza kodi ya mifugo, kilimo na mali. Tujiandae kisaikolojia kukamuliwa zaidi ya tunavyokamuliwa sasa.
Kumbe ndio maana wakati wa sensa wananchi walikuwa wanaulizwa thamani ya jengo, umiliki wa ardhi na mali nyingine kama vile mifugo, fenicha, nk. Ni kwa sababu hiyohiyo serikali ilitaka kufahamu kiasi cha ardhi wanacholima wakulima kijanja kwa kuwaahidi ruzuku ya mbolea kumbe ilikuwa danganya toto. Lengo halisi hasa lilikuwa serikali ipate takwimu halisi ili kila mtanzania alipe kodi kulingana na thamani ya mali anazomiliki. Nchi hii ni ngumu sana aisee!!!!
Tazama sasa serikali hii isiyokuwa na huruma ilivyokuwa na nia ovu ya kutaka kuwakamua wananchi wake bila kujali kwamba tayari wanaishi maisha ya kubahatisha kutokana na mfumuko mkubwa wa bei, gharama kubwa za kununua chakula na maji na kutopea kwenye ufukara. Hii nchi ni Mungu tu anayewaonea huruma wananchi wake. Lakini pamoja na kukamuana kote huku ipo siku Mungu atatenda muujiza kuwaokoa waja zake kutoka ugumu wa maisha wanayopitia.
Kumbuka hata nyakati zile wana wa Adamu wanaishi kwa shida kule Misri, Mungu alimtuma Musa kuwaongoza kutoka nchi ya utumwa hadi nchi ya ahadi waliyopangiwa na Mungu wao mwenye huruma. Basi kwa namna ya kipekee, tuendelee kuvumilia ndugu watanzania kwani Mungu yu karibu kurudi atukomboe kutoka minyonyoro ya utumwa wa watawala wa nchi hii wasiokuwa na chembe ya huruma kwa wananchi masikini.