Tozo ya uzalendo iendelee tu, tujikaze tujenge nchi

Yesu Anakuja

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2019
Posts
12,675
Reaction score
25,924
Kusema kweli toka moyoni, kama mzalendo, naamini tozo inatakiwa kuendelea, though ipunguzwe makali kama mama anavyosema, kwasababu tunahitaji pesa za kuendeshea nchi. Wote wanaopinga ni wale wanaotamani serikali isipate pesa iendelee kutegemea mataifa ya nje.

Pia, nitashangaa sana kama kuna mfanyakazi wa serikali hata mmoja anayepinga hii tozo, kwasababu pia itaboresha maslahi yao wanayolilia kila siku.

Wafanyakazi wanatoka kwenye familia zisizo za wafanya kazi pia, hivyo maisha yenu yakiboresha jueni hata maisha ya wasaio waafanyakazi majumbani kwenu yataboresha, ni njia mojawapo ya kujitegemea kwenye baadhi ya huduma kama nchi. Patauma lakini patazoeleka tu.

Tujikaze tujenge nchi.
 
Ahsante sana Rais wangu kwa msimamo THABITI kwa mwendo huu tutafika vizuri.

Nadhani wanao pima kina cha maji kwa rula bado hawajui kina vizuri.

Nafurahia sana makato haya yaendelee kama kawaida watazania wengi wanataka kero zao za maji, elimu, afya na miundombinu itatuliwe na sote tuko tayari kuchangia maendeleo yetu, marekebisho kidogo tu.

Kazi iendeleee.

Tulipe tozo kwa maendeleo yetu sasa wenyewe.

Mungu ibariki Tanzania
 
Ahsante sana Rais wangu kwa msimamo THABITI kwa mwendo huu tutafika vizuri.
nadhani wanao pima kina cha maji kwa rula bado hawajui kina vizuri.
imagine, tukitaka kufanya chochote, hata kujenga barabara vijijini, tunakinga bakuli kwa wazungu, wanakuja na masharti kibao, na wazungu wote hawaipendi CCM na viongozi wote wa serikali hii, mama asifikiri wazungu wanampenda, afanye mikakati ya kujitegemea kwenye vitu vya msingi.

Tozo ya uzalendo ni nafuu kuliko kodi ya kichwa ya zamani ambayo wazazi wetu walikuwa hawalali hata ndani, hii hapa unatoa kwa amani na inapatikana hela ya kutosha kujenga barabara, shule na kuendesha nchi. na kutapatikana hela ya kutosha sana kama tukishikilia msimamo huu huu.

Mimi binafsi sioni shida kukatwa hata alfu 30 kwa sababu huwa naweza kutoka na watoto wangu na familia na kuspendi hata 100,000 kwa siku moja kuwalisha tu mavyakula na vinywaji laini sasa kuichangia serikali alfu 10 ni shida? CDM acheni uhaini.
 
Tuko pamoja na Madam President..

Kuna watu wanamjaribu.. Amewaitikia wito wao na anawafundisha somo hivi sasa..

Sidhani kama atawaadhibu, just ni kuwafundisha somo tuu

KAZI IENDELEE.. MAMA ANAUPIGA MWINGI
 
kuna baadhi ya mikoa watoto wetu wa shule za misingi wanakaa chini kwa kukosa madawati halafu wanatokea watu wazima eti wanapinga tozo hii!! nasema kamwe tusikubali kuendekeza makelele. kazi iendeleee
 
Kusema kweli toka moyoni, kama mzalendo, naamini tozo inatakiwa kuendelea, though ipunguzwe makali kama mama anavyosema, kwasababu tunahitaji pesa za kuendeshea nchi. Wote wanaopinga ni wale wanaotamani serikali isipate pesa iendelee kutegemea mataifa ya nje.

Pia, nitashangaa sana kama kuna mfanyakazi wa serikali hata mmoja anayepinga hii tozo, kwasababu pia itaboresha maslahi yao wanayolilia kila siku.

Wafanyakazi wanatoka kwenye familia zisizo za wafanya kazi pia, hivyo maisha yenu yakiboresha jueni hata maisha ya wasaio waafanyakazi majumbani kwenu yataboresha, ni njia mojawapo ya kujitegemea kwenye baadhi ya huduma kama nchi. Patauma lakini patazoeleka tu.

Tujikaze tujenge nchi.
Nchi inawajinga wengi Sana hii ,mm nimekaa na pesa zangu tu yaan hali ikiwa hii nitafungua biashara nyingine
 
kiukweli kabisa, usalama wa watawala wetu ni muhimu unadhani ma v-8 yatafanyiwaje service? petrol za ma v 8? matibabu india? ni lazima watawala wetu walipwe vizuri wale washibe ili watuhudumie vizuri

UNAIJUA V 8 WEWE??
 
watu mnaogopa kulipa kodi? sisi wenzeni kila mwezi tunakatwa karibia laki tano kodi kwenye mishahara yetu, hatuogopi kulipa kodi, ni kwa maendeleo ya taifa. ukitaka kukwepa haya hamia burundi mzee.
 
kiukweli kabisa, usalama wa watawala wetu ni muhimu unadhani ma v-8 yatafanyiwaje service? petrol za ma v 8? matibabu india? ni lazima watawala wetu walipwe vizuri wale washibe ili watuhudumie vizuri

UNAIJUA V 8 WEWE??
somesha watoto waje wapande hayo mav8 au la nyamaza kimyaaa. duniani kote watawala huwa wanaishi maisha hayo, sisi sio kisiwa kwamba watawala wetu waishi kama manyani. kuna mengi wanafanya kwa ajili yako ndio maana hadi leo unabofya keyboard hapo kwa amani. ndezi kweli wewe.
 
mbona hasira si ndo nilichosema ndugu? unadhani babu tale ukimlipa chini ya laki 3 unadhani ataweza kuhudumia vizuri wana morogoro vijijini? ma v 8 nayo yanahitaji matunzo, ni lazima tuwatunze 'viongozi' wetu wanafanya mengi kwelikweli kwa ajili ya sisi mandezi
 
Acha upumbavu na kujitoa ufahamu
 
Acha upumbavu na kujitoa ufahamu
mkuu bajeti yetu huwa asilimia 80 ni matumizi na asilimia 20 ni kwa ajili ya maendeleo sasa bila sisi kulipa tozo za uzalendo matumizi ya viongozi wetu yatafanikiwa vipi? ni muhimu walipwe vizuri na kula vizuri na kutibiwa vizuri ili watusaidie kutuondolea shida zetu
 
Halafu kwenye kampeni za 2025 watuambie tumejenga barabara za vijijini na tumesambaza maji ilihali wananchi wenyewe ndio tumefanya hayo kwa njia ya tozo.
 
mkuu bajeti yetu huwa asilimia 80 ni matumizi na asilimia 20 ni kwa ajili ya maendeleo sasa bila sisi kulipa tozo za uzalendo matumizi ya viongozi wetu yatafanikiwa vipi? ni muhimu walipwe vizuri na kula vizuri na kutibiwa vizuri ili watusaidie kutuondolea shida zetu
😂😂😂😂😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom