Tozo za bila kufuata Sheria ni chaka la ufisadi

Tozo za bila kufuata Sheria ni chaka la ufisadi

Ndolezi Petro

New Member
Joined
Jun 26, 2024
Posts
4
Reaction score
1
Inauma, inasikitisha, inakera, Inaumiza, inasononesha na Inatia hasira, Serikali ya CCM ilivyo na mapuuza kwa raia wake.

Wameongeza Tozo kwenye LUKU kutoka 1500 kwenda 2000 kimyakimya bila kuwaeleza Watanzania. CCM haipaswi kuendelea kuongoza dola. ACT Wazalendo ni mbadala wa Uhakika
 
Kuna changamoto ambazo hatuzielewi sisi kama wananchi kuhusu ukusanyaji wa Kodi ya jengo kupitia "Luku", na Mimi naomba kupata ufafanuzi Kwa msaada pia wa wananchi wengine, yaani mimi nimekuwa nikinunua umeme Kila mwezi, na wanakata wakati mwingine hadi 6000 eti ni deni la pango, lakini Cha kushangaza zaidi Kila mwezi wanakata ninaponunua umeme, na haijalishi umeme umenunua hata Kwa mwezi mara mbili, ila wanakata Kila unaponunua, na zaidi Jana nanunua "LUKU" naambiwa deni langu ni kubwa, nikachukua jukumu la kupiga simu Tanesco, wakaniambia MITA yangu inadaiwa zaidi ya Tsh 20,000 na wakaniambia hawahusiki Kwa hilo, ila wahusika ni TRA lakini pia kupiga simu TRA nao wanasema hawahusiki, eti ni manispaa, na manispaa nawapigia simu nipate ufafanuzi namba naambiwa sio sahihi, hii inasikitisha sana Kwa wakazi wa Arusha jiji na maeneo mengine maana nimekutana na wafanyakazi wenzangu wengi wanalalamikia hii issue,
Ombi langu ni kwamba wakae chini wapitie mifumo yao, na waone shida Iko wapi, then watoe taarifa Kwa wananchi, yaani mtu una 10,000 unataka kununua umeme unapewa 2 units??
 
Back
Top Bottom