Tozo za kutuma na kutoa hela ni msumari mrefu kwenye paji la uso wa Mtanzania

Tozo za kutuma na kutoa hela ni msumari mrefu kwenye paji la uso wa Mtanzania

officialBossmtoto

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2019
Posts
370
Reaction score
1,189
Naomba nianze kwa kudeclare interest, mimi sina ushabiki na chama chochote cha upinzani. Wala sina itikadi ya chama chochote.

Tozo za makato ya kutumia mitandao ya sim sasa imepanda maradufu ukizingatia ni mda ambao serikali nyingi duniani zinatengeneza mazingira nafuu ya wananchi wake kufanya biashara kutokana na janga hili la Uviko-19.

Upandishwaji wa tozo hizi ni wazi kwamba umependekezwa, umekaguliwa na kuhakikiwa na watu wasio na huruma hata kidogo kwa watanzania wanyonge. Kuna mtanzania kila 100 yake ina faida na manufaa kwake.

Wapo ambao hata Gharama ambazo wengine tunataka zirejeshwe, kwao tayari zilikua ni mwiba.

Katika janga kama hili ambapo watu wanakaa majumbani kuepuka misongamano isio ya lazima, watu wanapunguzwa makazini kutokana na uzalishaji wa fedha kuwa mdogo, watu wanapoteza nguzo (nguvu kazi) za familia, ndo muda muafaka wameona kupandisha gharama za maisha kweli?

Jeshi linapambana na wezi mtaani na wakati kuna majangiri wanaovaa suti wanatumia elimu na nyadhifa zao kupora mali ya wavuja jasho. Hii tozo imewekwa kwa tamaa na haikua na mantiki ya kumuhurumia mtanzania hata kidogo.

Wangefanya hivi
Kwa miamala ya Tsh1000-tsh 9999 watu wakatwe shilingi 10 tuu. Kwa siku moja miamala ya kiwango hichi ni mingi sana. Kwa siku taifa litaingiza fedha nyingi tuu sana. Kama watu 1,000,000 tu kwa siku wangefanya miamala hii, taifa lingepata tsh 10,000,000 kwa miamala ya kiwango. Hiki.

Kwa miamala ya kuanzia tsh10,000-tsh99,000 wakate shilingi 100. Miamala hii pia ni mingi sanaa. Serikali bado itapata mahela mengi sana kupitia miamala hii. Kama kwa siku watafanya miamala hii watu 100,000 tayari serikali itakua imeingiza 10,000,000 zingine. Kwa siku.

Kwa miamala ya kuanzia tsh100,000 - tsh 999,999 serikali ikate 1,000 tuu. Hapa bado itavuna hela nyingi tu kutoka kwa watanzania. Na itazidi kupata loyalty ya watanzania wanaopenda nchi yao. Kama watanzania 10,000 tuu watafanya miamala hii, tayari serikali itakua imepokea fedha taslim shilingi 10,000,000 nyingine.

Kwa miamala ya tsh 1,000,000 na kuendelea serikali ichukue 3,000 tuu. Hapa bado itajipatia hela nzuri tuu kwa wananchi wake. Kama watanzania 5000 tuu watafanya miamala hii basi serikali itajipatia tsh 15,000,000 kwa siku hio.

Kwa haraka haraka kwa tarakimu hizo hapo juu. Basi wastani wa watanzania 1,115,000 watakua wamelichangia taifa wastani wa shilingi 45,000,000/ kwa siku.

Ila kumbuka kwamba mitandao ya simu sio chanzo pekee cha mapato serikalini hivo bado kuna hela nyingi sana zinakwenda serikalini kwa siku ukiachana na hii milioni 45,000,000, bado kwa siku watanzania wengi sana wanafanya miamala.

Serikali msigeuze raia wenu shamba la bibi. Mwisho wa siku mtakuja kututoza tozo za kuamka salama asubuhi.
 
Changia Tozo ya uzalendo kwa Maendeleo ya Taifa
Mkuu katika maswala hayabusifanye ubinafsi kujiangalia wewe una uwezo kiasi gani.

Kumbuka kuna mtu anaagiza nyanya na mboga mboga za kuweka gengeni kwake. Anatuma hela usiku ili asubuhi awahi kuchukua mzigo. Faida alikua anapata 15,000 tuu kwa siku. Leo makato haya yanaipunguza faida yake mpaka 9000. Hapo hajala hajalipia kodi watoto, hajawavisha na bado maisha sio siku moja ni kila siku.

Ni choyo ya hali ya juu kujifikiria wewe mwenyewe. Hujui mimi kama nina uwezo wa kulipa au la ila bado tozo hizo ni kubwa na unreal kwa watanzania wengi.
 
Mkuu katika maswala hayabusifanye ubinafsi kujiangalia wewe una uwezo kiasi gani.

Kumbuka kuna mtu anaagiza nyanya na mboga mboga za kuweka gengeni kwake. Anatuma hela usiku ili asubuhi awahi kuchukua mzigo. Faida alikua anapata 15,000 tuu kwa siku
Shauri zenu mnaotarajia muujiza
 
Mkuu katika maswala hayabusifanye ubinafsi kujiangalia wewe una uwezo kiasi gani.

Kumbuka kuna mtu anaagiza nyanya na mboga mboga za kuweka gengeni kwake. Anatuma hela usiku ili asubuhi awahi kuchukua mzigo. Faida alikua anapata 15,000 tuu kwa siku. Leo makato haya yanaipunguza faida yake mpaka 9000
Mkuu mi nimeongelea kishabiki tu mie pia ni maskini kama wewe tu tena hata kipato chako sina kwa siku!

Inaumiza sana hawa jamaa ni wabinafsi sana wamekalisha matumbo kwenye V8 ipo siku inatakiwa wapopolewe na mawe tu ili akili ziwakae sawa!
 
Mkuu mi nimeongelea kishabiki tu mie pia ni maskini kama wewe tu tena hata kipato chako sina kwa siku!

Inaumiza sana hawa jamaa ni wabinafsi sana wamekalisha matumbo kwenye V8 ipo siku inatakiwa wapopolewe na mawe tu ili akili ziwakae sawa!

Ipo siku mtanzania atachoka na dhuluma hizi, atachoka manyanyaso haya.
Nashindwa kuelewa viongozi tumewapa kura au kula?
 
Wanasiasa ambao watoto wao usoma shule za milioni 10 awafai kupewa kazi ya kuandaa bajeti
 
Back
Top Bottom