Tozo za kwenye vifurushi vya simu ziangaliwe upya

Tozo za kwenye vifurushi vya simu ziangaliwe upya

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2021
Posts
3,211
Reaction score
3,611
Kila ukinunua vocha na kuingiza kwenye simu ili usajili kifurushi unakumbana na tozo/makato ambayo ukija sasa kusajili kifurushi Mtandao unakwambia huna salio la kutosha kusajili kifurushi.

Nafikiri tarrifs za kusajili vifurushi ziangaliwe upya, mfano, vocha ikiwa na thamani ya Tshs.2000, ukiingiza serikali na taasisi zingine zinakata stahili zao labda jumla ya makato ni Tshs. 200, basi Mitandao iweke kwamba airtime/bundle itatolewa kwenye thamani inayobaki ya Tshs. 1,800 ili mteja asilazimike kununua vocha nyingine kwa ajili ya top up kupata Tshs.2000 wakati unakuwa na dharura na huna ela nyingine.

Tutendeane haki ili tusirudi kwenye zama zile za kuandika barua na kupeleka Posta.
 
Ni mambo ya kihuni sana yanayofanyika.Hii mitandao ishakua yaovyo.tunaishi kwakuvumilia tu.
 
Ni mambo ya kihuni sana yanayofanyika.Hii mitandao ishakua yaovyo.tunaishi kwakuvumilia tu.
Vocha zinatozwa, miamala ya kibenki inatozwa, miamala ya utilities km LUKU nk inatozwa! Uchumi mdogo (micro economy) unakufa, nafikiri tunahitaji kutafakari uamuzi huu upya.
 
Back
Top Bottom