NURURASHID
Member
- Jul 31, 2019
- 21
- 31
Katika Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa Fedha 2021/22 Serikali imedhamiria kukusanya mapato kutoka kwenye tozo za miamala ya simu, Tozo hizi ambazo katika macho ya watanzania wengi zinaonekana kandamizi na zisizo kubalika zilianza kutumika rasmi 15 July mwaka 2021 suala lilo zua mijadala ya namna mbalimbali na kupelekea serikali kutoa matamako mbali kuhusu tozo hizo Waziri mkuu, Waziri wa fedha na Rais wote katika nyakati tofauti tofauti walisema jambo kuhusu tozo hizo
Tatizo ni nini!?
Suala la kutafutia ufumbuzi ni kwanini wataalamu wetu wa kutengeneza mifumo ya Kodi (Tax Design) wanatengeneza Kodi isiyokubalika kwa walipa kodi kiasi hiki, je wataalamu wetu walifuata hatua za kutengeneza mifumo ya Kodi vizuri au walitumia kawaida na mazoea, Waziri wa Fedha katika mahojiano na chombo cha habari nchini aliseme tozo hizo zimeanzishwa baada ya kufanya uchunguzi na kujiridhisha vya kutosha ,Je wadau muhimu walishirikishwa katika kutengeneza Kodi ya miamala. Tozo hizi ni kandamizi kwa sababu zimeweka unafuu mkubwa upande wa benki na kufanya mazingira ya biashara ya uwakala kuwa magumu
Madhara ya Tozo za miamala kwenye uchumi
Tozo hizi zimeleta na zinatarajiwa kuleta madhara makubwa zaidi kwenye uchumi kama suluhisho la kweli halitapatikana, hapa chini ni miongoni mwa madhara hayo
1. Ajira; Watanzania wengi wamejiajiri katika biashara ya kutuma, kuweka na kutoa fedha maarufu Kama biashara ya uwakala, kuongezeka kwa gharama za kutuma na kutoa pesa kunamaanisha kudorola kwa biashara hii na hivyo kupelekea kufungwa kwa biashara na hatimaye kuongeza wimbi la ukosefu wa Ajira ambalo ni tatizo kubwa sana .Katika uchumi, katika uchunguzi usio rasmi uliofanyika maeneo ya Kawe kwa Joseph uligundua mawakala wameanza kufunga vibanda na kutafuta shughuli mbadala kwa sababu hawapati wateja
2. Kupanda kwa gharama za maisha. Tozo za miamala zimepelekea kupanda kwa gharama za maisha kwa sababu zimekuwa ni zaidi ya nusu ya gharama za kawaida za kutuma na kutoa pesa. Gharama ya kutoa zaidi ya milion 3 imekuwa mara tatu baada ya tozo hizi mpya
Chanzo: Vodacom Tanzania
3. Madhara katika Mzunguko wa Fedha, Huduma ya uwakala ilisaidia sana Mzunguko wa fedha, kwa kuwepo na hizi huduma kuliwezesha kutuma pesa kutoka maeneo ya mjini (zilipo benki mbalimbali) kwenda maeneo ya mbali (vijijini), kudhohofu na hatimaye kufungwa kwa biashara hii ya uwakala kutakuwa na athari hasi ya moja kwa moja kwenye Mzunguko wa fedha.
4.Kudorola kwa shughuli za uchumi, tangu kuanza na hatimaye kusambaa kwa huduma ya uwakala kulirahisisha ulipaji na ulipwaji katika shughuli nyingine za kiuchumi, ilikuwa ni rahisi mtu aishiye maeneo ya mjini kuendesha shughuli za kiuchumi vijijini mfano kilimo na kuwalipa wafanyakazi wake, wafanyakazi wakauza mazao na kumtumia fedha bila ya yeye kuwepo katika maeneo hayo, kudhohofu na hatimaye kufungwa kwa biashara ya uwakala kutamaanisha kudorola na kuanguka kwa shughuli hizi na hatimaye kudorola kwa uchumi
NINI KIFANYIKE
Ni wazi kuwa serikali ilikuwa na nia njema kuanzisha tozo hizo na kutenga mahususi mapato yatakayopatikana kutokana na tozo hizo (Ring Fencing) kwa ajili ya kujenga na kuendeleza barabara vijijini na hatimaye kukua kwa huduma za jamii na uchumi kwa ujumla wake lakni kiwango cha tozo hizo ni kikubwa mno kwa mwananchi wa kawaida (ambao hasa ndio watumiaji wakubwa wa huduma hizi)
Kwa hiyo serikali ipitie upya mfumo wa tozo na iwekee kiwango maalumu kwenye kila muamala kisichozidi Tsh 100 na itakuwa kwenye nafasi kubwa ya kukusanya mapato zaidi na kutimiza lengo lake
JE SERIKALI (MAMLAKA HUSIKA ) IMETUMIA IPASAVYO VYANZO VILIVYOPO VYA MAPATO KABLA YA KUBUNI CHANZO KIPYA!?
Jibu ni HAPANA vipo vyanzo vingi vya mapto ambavyo Mamlaka hajatumia vizuri kukusanya Kodi Kama ipasavyo mfano Kumekuwa na matakwa kwa mwenye jengo kuchukua Kodi ya Zuio (Withholding tax) sawa na 10% ya gharama ya Kodi ya nyumba Kisha kupeleka kiasi hicho TRA, je ni wenye nyumba wangapi hulipa Kodi ya Zuio TRA. Achana na Kodi ya zuio, ni wafanya biashara wangapi hawalipi kodi ya mapato itokanayo na biashara katika hasa maeneo ya vijijini, jibu ni kwamba wafanya biashara wengi maeneo ya vijijini hawalipi kodi ya mapato na siyo Kama hawapendi kulipa lakni TRA haijawafikia, ofisi za TRA zipo katika makao Makuu ya mikoa na wilaya tofauti kwenye majiji Kama Dar es salaam.
Tulitakiwa kuhakikisha kwanza tunatumia vizuri vyanzo vilivyopo kabla ya kubuni chanzo kipya (Tozo za miamala ya simu)
Imeandikwa na
Nuru M Rashid
Mchambuzi Masuala ya Kodi na Uchumi.

Upvote
3