Tozo za miamala na Masoud Kipanya

Tozo za miamala na Masoud Kipanya

nusuhela

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2014
Posts
5,915
Reaction score
7,210
Hili suala la tozo limekua na mguso mkubwa sana kwa watumiaji wa miamala ya fedha kupitia mitandao ya simu za mkononi.

Ni vilio kila kona na nyuso zisizo na furaha. Kila mmoja analiongelea hili suala. Sio mtandaoni na wala sio uswahili kwetu. Kila mmoja analalamika na kunung'unika kivyake kwa kiasi kikubwa kinachotozwa na serikali kupitia miamala.

Mbaya zaidi ni kuwa taratibu zote za upitishwaji wa sheria wa tozo hizi mpya, zilifuatwa mpaka mh rais akatia sahihi yake kupitisha.

Baada ya tozo hizi mpya kuanza kutumika mnamo tarehe 15 july 2021, kila mtu alionyesha kupinga vikali tozo hizi kwakua ni kandamizi kwa mtumiaji.

Wengi waliuliza uhalali wa tozo hizi maana ukituma na kutoa fedha, unakatwa kiasi ambacho hata makamapuni ya simu hayatozi kiasi hicho kama ada ya miamala..

Wengi wetu tukaamua kuachana na huduma hizo maana sio maji wala chakula kuwa usipokunywa au kula, utaukosa uhai wako.

Matamko ya waziri wa fedha ya kusema "tutazoea tu", yalitukatisha tamaa na kuanza kuona mwisho wa huduma hizo.

Baada ya siku kadhaa tangu kuanzishwa kwa tozo hizo mpya, baadhi ya makampuni yalianza kulalamika kukosa wateja hasa maeneo ya vijijini. Ndipo serikali ilipoanza kushtuka kuwa hawatakosa tozo tu, bali watakosa na kodi walizokua wanakusanya hapo awali kutoka kwenye ada za miamala ya fedha.

Tumeanza kusikia wanaanza kupeana maelekezo ya kuliangalia upya suala hili.

Hii ndio ile kampa kampa tena na masoud kipanya kuhusu tozo mpya
View attachment 1860357
 
Sasa hata kama watasitisha hiyo tozo watakuwa wamepata fedha si kidogo kwa muda huo. Na ikisitishwa tozo hiyo huyo waziri wa fedha hana budi kujiudhuru kama ishara ya kushindwa kuwajibika kiuweledi namna ya kubuni tozo zisizowaumiza wananchi.
 
Ngoja tuone....movie itakapoishia huyu Masoud Kipanya si alitekwa siku mbili huyu na wasiojulikana?
 
Nchi inategemea kilimo harafu wameongeza kodi kwenye pembejeo huyu Mwigulu kazi imemshinda aachie ngazi...
 
Back
Top Bottom