Tozo za miamala ya simu ni kikwazo kwa biashara ndogo

Tozo za miamala ya simu ni kikwazo kwa biashara ndogo

Bozi

Member
Joined
Oct 13, 2012
Posts
92
Reaction score
144
Kama kuna mahali serikali hii imekosea ni kuhusu hii tozo ya miamala ya simu, madhara yake yatakuwa makubwa sana kwa biashara za watu wa chini. Wafanyabiashara wadogo wengi hawatumii bank kufanya manunuzi na malipo mbalimbali.

Tozo iliyowekwa ni kubwa kuliko faida tarajiwa katika muamala husika. Miamala mingi inafanyika kwa ajili ya kurahisisha tu kazi za watu lakini yenyewe haina faida hata iweze kumudu kulipa tozo kubwa namna hii. Wafanyabiashara wakubwa wanafanya biashara kupitia miamala ya kibenki, hawatumii miamala ya simu, kwa kiasi kikubwa huduma hii ni kwa ajili ya watu wa chini.

Ni kitu gani kimeifanya serikali ifikiri huku kutaleta mapato makubwa na kusahau athari zake. Huduma hii imekuwa kichocheo cha sekta zingine nyingi, kuifinyanga namna hii haiumii sekta hii peke yake bali unaathiri sekta nyingi za kiuchumi ambazo huduma hii imekuwa mwezeshi.

Hizi ni athari za hii tozo kwa mtazamo wangu;
1. Biashara ya fedha kwa simu itaathirika na ajira nyingi zitakufa kwa kukosa wateja
2. Wafanyabiashara wadogo ndio watakuwa waathirika wakubwa
3. Kasi ya mzunguko wa fedha kwenye uchumi itapungua sana
4. Watu wengi wataanza kutembea na cash na matumizi ya cash yatarudi kwa kiasi kikubwa.
5. Kampuni za simu zilizowekeza kwenye biashara hii zitaathirika sana
6. Kasi ya uchumi itapungua kufuatia kupungua kwa kasi ya shughuli za uzalishaji.

Ni vema serikali kama inataka mapato basi itambue ni kiasi gani cha tozo kinapaswa kutozwa pasipo kuathiri/kuua kabisa sekta nzima.

TOZO HII KUBWA MNO HAIBEBEKI NA HAINA UHALISIA NI MATESO MAKUBWA KWA WATU WA CHINI
 
Watanzania tutazoea tu ingekua ni Afrika Kusini kuna shoti ingetokea
 
Nchi yetu itajengwa na sisi tukubali hivi sisi si tunajinasibu tupo uchumi daraja la kati? Au la kati kinadharia tu?

Kama mtu anafanya biashara haimlipi ningeshauri tu afanye biashara nyingine ambayo inalipa.
 
Hii ni nchi yetu sote si nchi ya watawala, wadhalimu wakubwa

Wananchi wa hali ya chini ndio kipaombele kwa serikali zote zinazofuata haki, uwajibikaji na Sheria

Serikali hii ambayo haijali maoni ya wananchi wake, huku wao wananeemeka na mishahara na marupurupu makubwa na hawakatwi Kodi halafu wewe unashupaza kende zako halafu unatetea ujinga
 
Yaani ni kama unatumia pesa watu wawili unaitumia pesa serikali na kwa yule unaemtumia! Tatizo ni kiasi kingi mno[emoji22][emoji22][emoji22][emoji22][emoji22]
 
Nchi yetu itajengwa na sisi tukubali hivi sisi si tunajinasibu tupo uchumi daraja la kati? Au la kati kinadharia tu?

Kama mtu anafanya biashara haimlipi ningeshauri tu afanye biashara nyingine ambayo inalipa.

Wewe ni mnufaikaji katika hili, kama ni mbunge basi uzi huu haukufai. Na hujui biashara ni kitu gani au ni mtu tu unakaa kwa shemeji.
 
Nchi yetu itajengwa na sisi tukubali hivi sisi si tunajinasibu tupo uchumi daraja la kati? Au la kati kinadharia tu?

Kama mtu anafanya biashara haimlipi ningeshauri tu afanye biashara nyingine ambayo inalipa.
Bila shaka hufanyi biashara na wala hujawahi, mawazo yako ni nje ya muktadha.
 
Back
Top Bottom