Tozo za miamala zitakuwa zimegusa stahiki za Wabunge? Mwigulu mbona hilo hujalizungumzia!

Tozo za miamala zitakuwa zimegusa stahiki za Wabunge? Mwigulu mbona hilo hujalizungumzia!

Ss Jr

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2018
Posts
577
Reaction score
451
Thadei Ole Mushi
TUSIFUNGE MJADALA WA MSHAHARA WA MBUNGE.
Na Thadei Ole Mushi.
Kuna Msaidizi mmoja wa Mbunge Kanitumia document hizi ili kufanya Clarification zaidi kwa jamii kuhusu Mishahara ya Mbunge.
Twende sawa hapa.

1. Mbunge hulipwa mshahara kwenye scale ya LSS (P) 2 ambayo mshahara wake ni Shilingi 4,600,000.

2. Atalipwa posho ambazo kwa Mwezi hufikia Shilingi 8,292,000 katika mchang'anuo ufuatao.

✓ Atalipwa posho Kwa ajili ya mafuta ya gari yake Shilingi 3,750,000.

✓Atalipwa Posho Kwa ajili ya Matengenezo ya Gari yake Shilingi 1,500,000.

✓Atalipwa Posho inayoitwa (Posho ya Mbunge na matumizi mengine jimboni) Shilingi 1,000,000.

✓ Atalipwa Posho ya kujikimu ya siku 10 kama atajisikia kwenda Jimboni Shilingi 450,000.

✓ Atalipwa Posho ya kujikimu kwa Wasaidizi wake watatu Kwa siku kumi atakazokuwa jimboni Shilingi 900,000 hapa kama atajisikia kwenda Jimboni au kwa mchepuko Dar

✓ Atalipwa Posho ya watumishi watatu kama atajisikia kuajiri (Mhudumu wa Ofisi yake, Katibu wake, na Dereva) katika mchang'anuo ufuatao.

Katibu wake Shilingi 352,000 Mhudumu 170,000, Dereva 170,000. Jumla Shilingi 692,000. Hapa ni kama atajisikia kuajiri sio lazima.

Jumla ya Fedha zote zinafika Shilingi 12,892,000.Fedha hizi zote zinaingia kwenye account yake Mbunge.

Ukiwahoji wanasema mshahara wao unabeba Mishahara ya wasaidizi wao ndio maana unaonekana mkubwa. Kwenye huo mshahara na posho zake ukitoa Mishahara ya wasaidizi watatu niliokutajia hapo juu anabakia na Shilingi 12,200,000. Hapa atakuwa ameshalipa Watumishi wake watatu wote Stahiki zao kama atakuwa kawaajiri kweli.

Na ninyi ni mashahaidi Hawa watu hawana Watumishi ambao ni wasaidizi wao ni wachache Sana ambao wanao.
Mtumishi mwingine wa Umma analipwa Mshahara wake wa Laki Tano ambao atatengenezea pikipiki yake, ataweka mafuta pikipiki yake, atalipia House Girl wake na atalipia ada watoto wake.

Hii sio sawa hizi Posho ni nyingi mno zinapaswa kupunguzwa. Wananchi wanapaswa kufahamu anacholipwa Mbunge wake na alinganishe na Kazi anayoifanya.

Qualification ya kuwa Mbunge Kujua Kusoma na Kuandika.
Share na wananchi wa majimbo Mengine... Ushahidi huo hapo.
Ole Mushi
0712702602.
FB_IMG_16247422236504968.jpg
View attachment 1855617View attachment 1855616
 
Hizo posho nimezisoma ikabidi nitabasamu tu, halafu mnasema mpaka leo hatumjui adui yetu, na chanzo cha umaskini wetu.
Nahisi umepitia haraka haraka ebu pitia tena kwa umakini halafu mtaarifu na mwenzako
 
Haya malipo kweli ni madogo sana. Ni vizuri wakaongezewa zaidi maana wao ni wazalendo mno.

Halafu hizi tozo za uzalendo kwetu bado ziko chini sana. Ilikuwa vizuri ziongezwe zaidi.

Kwanza wenzao wanalipwa kwa US $.

Mh. Zungu simamia hilo tafadhali.
 
Back
Top Bottom