CM 1774858
JF-Expert Member
- May 29, 2021
- 5,621
- 5,029
Tozo za miamala ya simu zitasaidia ujenzi wa Shule zaidi ya 10,000; Zahanati zaidi ya 4,500 na vituo vya afya 570 ifikapo 2025, Uzalendo zaidi unahitajika kwani vizuri vinamaumivu,
Tupige moyo konde, nikweli pesa hakuna,nikweli mzunguko wa pesa si mzuri sana ila tuwaache wenye pesa walisaidie Taifa lao kwa faida ya watoto leo na faida ya watoto wao kesho.
Tuacheni harakati kwenye maendeleo ya watu, hayupo Mjomba wala shangazi wakutujengea hizi barabara, shule,Zahanati,Hospitali kwaajili yetu na kwaajili ya watoto wetu na watoto wao ila ni sisi wenyewe.
[Hebu angalia faida za tozo kwenye sekta mbili tu za Afya na Elimu]
1. UJENZI WA VYUMBA 8,000- 10,000 VYA MADARASA VIPYA
Tunaweza kujenga shule 2,000 za O'level au shule 2,500 za A'level au Shule 1,428 za kidato cha ( I-VI) au Shule 1,250 za Msingi hii ni sawa na katika kila kata 2 itajengwa shule mpya 1 kwenye kata zote 3,956 au nisawa nakusema katika kila jimbo la uchaguzi kwenye majimbo yote 264 zitajengwa shule mpya 8 za Mama Samia likiwemo Jimbo la kaka yangu, "Thadei Ole Mushi " anayezipatia kigugumizi hizi tozo ,Nakwarejea tu,Tanzania tuna shule 5,330 tu za sekondari,Shule mpya nikaribu nusu ya shule zote za sekondari zilizowahi kujengwa tangu Uhuru kwanini tuendelee kunung'unikia tozo Kila siku tozo,
Nakama tozo hii itaenda mpaka 2025 Mama Samia atajenga shule mpya zinazofikia 10,000 hii ni sawa na kusema karibu kila kijiji kitakuwa na shule mpya ama ya sekondari ama ya msingi kupitia tozo za e-money.
2. UJENZI WA ZAHANATI MPYA 900
Hyt Rais Magufuli kwa miaka mitano alijenga Zahanati 1,198.Leo Mama Samia kwa kutumia Tozo ya Uzalendo atajenga Zahanati mpya 900 kwa mwaka 1 wa fedha yaani FY 2021|22.Hii ni sawa na Zahanati mpya 4,500 kwa miaka 5 yaani kila Jimbo zitajengwa Zahati mpya 4 katika kila mwaka wa fedha ni sawa na Zahanati 20 kwa kila jimbo kwa miaka 5 ya kwanza ya Mhe Samia Suluhu na hii ni kwamajimbo yote 264,Kwa lugha rahisi ifikapo 2025 kila kata itakuwa na Zahanati Mpya 2 za Mama Samia Suluhu Hassan,
3. UJENZI WA VITUO 234 VYA AFYA
Hyt Rais Magufuli kwa miaka 5 alikarabati na kujenga jumla ya vituo vya afya 487,Leo Mhe Rais Samia Suluhu kwa kutumia Tozo ya e-money atajenga vituo vipya 234 kwa mwaka 1 huu na nusu sawa na vituo 570 kwa miaka 5 ya awamu ya kwanza,Kwa lugha rahisi mwaka 2025 kila Wilaya itakuwa na Vituo vipya 4 vya afya vya Mama Samia Suluhu Hassan vitakavyohudumia watoto wa masikini wa nchi hii,
Itaendelea, kazi iendelee...