Tozo za miamala zitasaidia ujenzi wa Shule zaidi ya 10,000; zahanati zaidi ya 4,500 na vituo vya afya 570 ifikapo 2025. Uzalendo zaidi unahitajika

Bado Watanzania tunahitaji kumwomba Mungu alisaidie Taifa letu!
 
Siasa mbaya Sana ,ikifika 2024 pesa hizo hizo za wananchi zitafanya kampeni na kununua wapinzani na kuhonga watu .
Sisiem ni ileile mark ma words
 
Unataka kutuaminisha kuwa bila hizi tozo hakuna maendeleo?
Kwani waliojenga hizi tulizonazo walitumia hela gani?

Acheni kuwaibia wananchi kwa kusingizia kuwapelekea maendeleo wakati wanalipa kodi lukuki ambazo ndizo zilizotakiwa kuwapelekea hayo maendeleo..

Hizi tozo mpya naita ni unyang'anyi..

Pili zinafanya mzunguko wa miamala kuwa mdogo.
Mzunguko wa miamala ukiwa mdogo maana yake tunaongeza wimbi la ukosefu wa ajira maana mawakala wengi watafunga kwa kukosa wateja.

Miamala sio chakula kuwa lazima watu watakula tu, ni hiari ya mtu kwenda kupoteza hela yake mwenyewe. Hivyo wengi wameamua kusitisha huduma hiyo maana tozo sio rafiki kwa watumiaji.

Tatu makampuni ya simu yatapata hasara ambayo itapelekea serikali kukosa kodi ambazo ilikua inakusanya kutoka kwao. Hii itasababishwa na mzunguko wa miamala kushuka kwa kasi....

Hizi ni hesabu zangu ambaye hata form four sina. Alafu eti tuna waziri, makamu wa raisi na raisi ambao ni wasomi wa uchumi...

Labda uchumi wa maganda ya korosho
 
Unalinganisha na nchi ipi ambayo Wafanyakazi wake hawajaongezewa mishahara kwa miaka sita!? Wakulima na Wafanyabishara wanadhulumiwa hadi Wafanyabishara wanaikimbia nchi ili wakafanye biashara nchi nyingine!? Hebu acha KUDEMKA!!!


 
Kaingia cha kiume....
 
Katika watu ambao ni wapuuzi basi ni Hawa viongozi wa sasa, yaani badala ya kutoka kuwaeleza watu tozo hizo zimewekwa kwa ajili gani na zitafanya nini yamekaa kimya yanawaacha machadema yanatamba.

Wanao umia kwenye kukosa hizo huduma ni hao hao wanaojiita maskini ndio watoto wao wamerundikana kwenye madarasa,ndio hawana bima na wanazalia chini kwenye hospital chache zilizopo,hawana maji na mbaya zaidi barabara za uhakika hakuna.

Hao ndio Mtaka aliwaambia watoto wao wanatembea km 50 zaidi kwa wiki ila hawataki kuumia sasa ngoja waendelee kusugua zaidi tuone kama wakibaki na hivyo vihela watatoka kwenye umaskini.

Unawasikiliza wapuuzi wa CDM hawajawahi Jenga shule hata moja ya mfano kusaidia jamii wanaishi kwa ruzuku za serikali na misaada ya wazungu,wewe unaehaso eti unacheza ngoma yao?
 
Siasa mbaya Sana ,ikifika 2024 pesa hizo hizo za wananchi zitafanya kampeni na kununua wapinzani na kuhonga watu .
Sisiem ni ileile mark ma words
Acha ujinga ni wajibu wa kudai waoneshe hivyo vitu hapo juu sio kuitikia feelings tuu
 
Usiwe mjinga kwa miaka 6 iliyopita mfano Magu kajenga vituo vya afya 300 na hospital 60 tuu na hadi anakufa karibu vyote havifanyi Kazi hakuna pesa za umaliziaji.

Na bado nahitaji mengine kibao kwenye sekta zingine inamaana tukiendelea kujivuta vuta tutafika miaka 100 ya uhuru hakuna cha maana nchi imefaulu si barabara si elimu si afya .

Matokeo yake ni umaskini zaidi kwa wale mbaiwatetea saizi na bahati mbaya hii nchi kasi ya uzazi ni kubwa Sana.Fikiria kwa mfano Mji wa Tunduma una zaidi ya wakazi 200,000 lakini ina kituo cha afya cha serikali 1 tuu huku hospital iliyoanza kujengwa awamu ya mwendazake haijulikan itaanza lini Kazi.

Ukipata changamoto ya Afya usafiri kwenda Wilaya zingine hizo gharama unaziona? Kipi bora hapo kulipa tozo kwa mda Ili kupunguza changamoto au kuendelea kulialia huku ha
 

Wekeni jedwali kwanza la hospitali na vituo vya afya vilivyojengwa wakati wa magufuli, mahali vilipo na thamani yake. Msitutajie idadi peke yake mkadhani sisi ni wajinga wa hivyo. Tunataka tujue hizo hospitali, shule nk mnazotaja mnataka kuzijenga wapi na thamani yake, ili tupime hiyo hela itaingia wapi na lini ni mwisho wa hayo makusanyo.
 
Mbona unaongea kinadharia sana . Wanakatwa mamilioni kwenye nn? Kwenye faida wanayoingiza ama kwenye mitaji yao? Ukijua hili utajua nn watu wanalalamikia
 

Makato sasa mkajengee mahekalu wastaafu na kuwapa magari wakati hawana uhitaji huo wala tija yoyote? Hayo makusanyo sio ndio mnawazungushia wastaafu kwenda kwenye miradi ambayo aliwashinda kujenga? Kama mnadhani kuna mjinga mtamtajia idadi ya hospitali na shule bila kutaja ni wapi na thamani ya hiyo miundombinu basi mmechelewa. Kauzeni zile rasilimali Magufuli alizokuwa analinda, kisha mjengee hivyo vituo vya afya.
 
Unatumia hisia kuniaminisha kuwa kuipa serikali hela zaidi ya inayostahioi kukusanya ndiko kutakakoleta maendeleo.

Acha nikuulize haya maswali na ninaomba unijibu kwa ufasaha kisha nitakuelewa kuhusu hizi tozo

1. Hela za kununua ndege zilitoka wapi?
2. Hela za kujenga kiwanja cha ndege chato zilitoka wapi?
3. Hela za kununua ma-V8 zinatoka wapi?
4. Hela za posho za wabunge zinatoka wapi?
5. Hela za per diem zinatoka wapi?
6. Hela za kujengea wastaafu nyumba zinatoka wapi.?

Mimi nadhani kama taifa hatuna vipaumbele. Viongozi wapo ili kujinufaisha wao na familia zao. Wala sio eti hakuna hela za kuboresha huduma za muhimu kwa wananchi..

Hapo wameongezea hizo tozo ili wapate hela ambazo hazikusanywi na TRA na hakuna atayehoji imekunywa ngapi. Hapo ndipo watakapo tajirikia.

Umewahi kujiuliza ni nini faida ya
1. Bandari tulizonazo
2. Madini
3. Mlima kilimanjaro
4. Gas ya mtwara
5. Kodi zinazokusanywa kila uchwao
6. Mbuga za wanyama

Na mengine mengi kwa mtanzania wa kawaida?

Kwa taarifa yako, hizo tozo zinaenda kuleta mdororo wa mzunguko wa miamala kiasi kwamba badala ya kupata, watapoteza hata ile VAT waliyokua wanaipata kupitia ada ya miamala.

Watu wa aina yako ndio wanaotoaga ushauri wa kuangamiza taifa kwa kujifanya wajuaji kumbe ni mburula wa mwisho
 
Haya ni mahesabu tu ya kwenye makaratasi tukirudi kwenye uhalisia hilo jambo halitawezekana.

Watanzania ni wazuri sana kwa mipango ila utekelezaji hapana.

Kwa bahati mbaya hizo fedha zitaingia kwenye mifuko ya watu kama nyingine tu.

No guarantee.
 
Huyu mama anahesabu kali sana huenda akavunja rekodi kwa ujenzi wa miundombini ya maendeleo kwa wananchi.

Japo makato yanauma ila kama mambo ni haya niko tayari.
Uko tayari kufanyaje?
Maneno mepesi tu umeshaingia mtegoni.
Hizo ni fix za wanasiasa...watanzania tujifunze kuwahoji sana hawa watu.
Walishatudanganya mengi.

Walitudanganya Gas ya Mtwara ikikamilika umeme utashuka bei...yako wapi?!
 
Ndoto za Alinacha hizo. Anapiga hesabu ya vifaranga atakavyopata, idadi ya kuku kutokana na hao vifaranga na fedha atakavyopata baada ya kuwauza hao kuku. Kasahau kabisa kwamba mayai bado hayajaanguliwa.
 
Nitumie hisia Ili iweje ,wewe ndio unaongozwa na hisia za kipuuzi ukiwa na mentality ya kipuuzi pia kwamba pesa inaibiwa.

Kwanza lazima uelewe pesa ya kuendeshea Serikali lazima ipatikane iwe ni per diem,salary,sjui posho za wabunge au kununua magari ya serikali lazima popote itakapopatikana hayo ndio mambo ya kwanza Ili ku run serikali na ku restore order.

Pili pesa ya maendeleo ndio haitoshi na ndio inatafutwa kwa vyanzo vingine ikiwamo kodi na tozo nk.

Madini unayotaja wewe yanahitaji wawekezaji kama mnavyowekeza kwingineko na aliyewekeza ndio anapata pakubwa kwa hiyo hujakatazwa kuwekeza ila mtaji huna na kama huna yakiendelea kukaa ardhini ni useless .Kwa taarifa yako tozo za madini yote uyajuayo nchi hii huipatia serikali chini ya bln 600 kwa hiyo usiwe obsessed na kitu madini sio valuable kwa kiwango unachofikilia wewe.

Hizo bandari bila miundombinu ni useless ni sawa tuu na kuwa na madini au mali nyingine ila huna uwezo wa kuvigeuza kuwa pesa au hata ukijitahidi Unapata kiduchu Sana.

Na nchi hii ina watu wengi mnazaana Sana na mahitaji yanakuwa daily kwa hiyo bila kujikamua umaskini utazidi kutamalaki.Na hao unaojifanya kuwatetea huwasaidii ila ndio kwanza watazidi kudidimia kama Serikalini isipochukua hatua kali kama hizi kuwainua hao watu.
 
Sasa mbona sijakuelewa. Kwahiyo kipaumbele chetu ni hayo magali, posho, per diem na huo ushubwada na sio huduma bora kwa wananchi si ndio?

Hivi si ndio nyie mnaotaka kujenga sanamu kwa kodi zetu?

Si ndio nyie nyie mnao jengeana nyumba wastaafu kwa hizo hizo kodi mnazoona hazitoshi?

Yaani mnatumia hela hovyo kufanya matumizi yasiyo ya lazima tena hela zetu alafu mnakuja mnataka nyingine wakati hizo mnazokusanya hamtuletei yale mnayotuahidi mpaka tunaona sawa tu kukatwa kodi.

Au mnadhani kodi mnayokata ni fungu la kumi? Ni hela zinazotakiwa zipelekwe moja kwa moja kwenye maendeleo na sio kujilipa maposho ambayo mnakaa kujadili vitu ambavyo havitekelezeki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…