Tozo za miamala zitasaidia ujenzi wa Shule zaidi ya 10,000; zahanati zaidi ya 4,500 na vituo vya afya 570 ifikapo 2025. Uzalendo zaidi unahitajika

hakuna asie taka kulipa kwanini wabunge na viongozi mbali mbali hawakatwi? kama kweli ni uzalendo na wao wakatwe
 
Wazo zuri ila sio kugomea tozo, zitumikaje ni mjadala mwingine
 
Hizo namba ni rahisi sana kusomeka,kiutendaji hakuna kitu cha hivyo.
Tunayo mifano hai mingi tu ...
 
Huyu mama anahesabu kali sana huenda akavunja rekodi kwa ujenzi wa miundombini ya maendeleo kwa wananchi.

Japo makato yanauma ila kama mambo ni haya niko tayari.
Punguza ujinga: kama nia ilikuwa njema wananchi walipaswa kujua mnakadiria kupata shilingi ngapi? Kwa muda upi? Na je mgwanyo wa matumizi utakuwaje kwa kila halmashauri.
Waambieni vile vile nini kitafuata endapo mambo yataenda ndivyo sivyo!
Tukumbuke kuwa hii ni tozo ya hiyari siyo kodi ya lazima. Wapo ambao watagoma kuilipa kwa kuacha kutumia mitandao ya simu na hakuna mtakacho wafanya!

NB: mngepata hela nyingi endapo mngeamua kusitisha manunuzi ya magari ya kifahari kwa pesa za wananchi hao hao mnao rudi kuwakamua!
Mmetapeli mengi; sidhani kuwa mna nia njema!
 
Wapunguze matumizi serikalini, hasa kwa viongozi, misafara, safari za nje, magari yenye gharama n.k.
Wabunge waongezewe kukatwa kodi..
 
Umefuatilia hii ukaambiwa hakuna unachokizungumza?
 
Tozo kwa ajili ya kulipana posho, kuua upinzani, kuwafanya watz wawe masikini zaidi. Kuiba na kufanya ufisadi, kuvuruga uchaguzi,

Hatutumii miamala si mnasemaga hii nchi tajiri, tafuta vyanzo kwenye madini, na gesi
 
Hii nchi utadhani inawakazi wa kukodi yaani,

Kila kitu kwao kibaya
 
Hii nchi utadhani inawakazi wa kukodi yaani,

Kila kitu kwao kibaya
 
Sio tatizo, je zitajengwa ama zitaishia matumboni mwa watu?
 
Nadhani hii thread ingefutwa tu sababu hata tozo zenyewe zimefutwa. Huu upupu hauna ishu
 
Point
 
Mama akigusa wabunge tu kwenye hili afwile!
 
Nadhani hii thread ingefutwa tu sababu hata tozo zenyewe zimefutwa. Huu upupu hauna ishu
Tozo zinaendelea na lazima haya yafanyike kabla ya 2025,

Tanzania itachengwa na Watanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…