robinson crusoe
JF-Expert Member
- Oct 22, 2020
- 762
- 1,236
Huu ndo unyonge wa mwafrika. Badala ya mambo muhimu ya elimu, Wairi Ummy anajigamba kununua magari ya maafisa elimu. hizo ni pesa za wa-TZ zinatumika kununulia magari ya anasa Japan. Mashuleni hakuna madarasa, hakuna maabara, hakuna nyumba za waalimu. hakuna mabweni na hata madawati bado ni changamoto. Mishahara ya waalimu ni hovyo kabisa, halafu waziri anapanga kuwatafutia usafiri wa serikali, ili iweje? Wakistaafu watakwenda na nyumbani na usafiri?
Ni aibu sana kuwa na viongozi dhaifu kwa kiwango hiki! Viongozi wasiojua elimu ni nini! Yaani hata magari tumeona ni kifaa cha kuinua elimu nchini?
Ni aibu sana kuwa na viongozi dhaifu kwa kiwango hiki! Viongozi wasiojua elimu ni nini! Yaani hata magari tumeona ni kifaa cha kuinua elimu nchini?