Tozo za Simu zinakiuka katiba

Tozo za Simu zinakiuka katiba

Kasomi

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
11,030
Reaction score
20,391
TOZO ZA SIMU ZINAKIUKA KATIBA YA NCHI

Viwango vipya vya tozo za mihamala vinakiuka katiba ya nchi. Iwe Katiba ya Sasa, Katiba mpya pendekezwa au ile ya Warioba. Zote zinakanyagwa kwa njia hizi:

1. Vinaingilia uhuru wa kuwasiliana. Uhuru wa kukusanyika siku hizi unafanyika kwa kuwasiliana. Watu wanalazimika kutowasiliana. Katiba inatoa uhuru, tozo zinauondoa.

2. Tozo hizi zimeunganisha mihimili miwili (bunge na serikali) dhidi ya wananchi na walaji. Katiba inatenganisha mihimili hii miwili. Tozo zimeiunganisha. Ni kinyume cha katiba. Wabunge wamekubaliana na serikali kuwanyonya wananchi. Nani mtetezi wa wananchi?

3. Tozo zinaondoa usalama wa watu na fedha zao. Watu wanalazimika kutumia "cash" badala ya kutuma kwa njia ya mitandao. Watu wanalazimishwa waonekane wanatakatisha fedha au kuhujumu uchumi. Serikali inashirikiana na mitandao ya simu kuhujumu na kutakatisha fedha.

4. Katiba inatamka kuwa mamlaka ya bunge na serikali inatokana na wananchi. Bunge na serikali ni watumishi wa wananchi. Tozo hizi zinabadili mtiririko huu na kuifanya bunge, serikali na makampuni ya simu kuwa juu ya wananchi. Huu ni "uhaini" dhidi ya mamlaka ya wananchi.
 
IMG_20210715_213635_704.jpg
 
Mama ni muislamu kaamua kushiriki dhuluma kupitia wizi wa kuwapora wananchi kupitia tozo hizi za dhuluma zilizopo Tza pekee duniani nzima Hakuna tozo kama hizi.
 
Tupaze sauti Wabunge wawe chini yetu. Katiba mpya tu hakuna jinsi.
Ccm hawawezi kukubali kua na katiba mpya hofu yao wataondoka madarakani, na bahati nzuri watanzania ni makondoo hayawezi kuongea
 
Litakaukiwa hadi maji safari hii😂😂😂😂😂😂
 
Mama ni muislamu kaamua kushiriki dhuluma kupitia wizi wa kuwapora wananchi kupitia tozo hizi za dhuluma zilizopo Tza pekee duniani nzima Hakuna tozo kama hizi.
Kauli za kijinga hizi ni kama jinamizi hivi,kuitwa juma,rajab,peter,angel hakukufanyi uwe na tabia au maadili mazuri.
 
Back
Top Bottom