Tozo za simu zingetumika kutengeneza Mfuko wa Bima ambao ungekuwa maalumu kukabiliana na corona nchini

Tozo za simu zingetumika kutengeneza Mfuko wa Bima ambao ungekuwa maalumu kukabiliana na corona nchini

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Kabla hata Zungu hajapendekeza Bungeni kodi kwenye miamala ya simu, mimi nilileta wazo kupitia hapa JamiiForums nikipendekeza tozo kupitia line za simu zitumike kuunda Mfuko wa Bima ya Afya kwa kila mtanzania atakaekuwa tayari kuchangia bima hiyo kupitia line yake ya simu.

Nilipendekeza namna ya kuunda huo mfuko, namna ya kuuendesha na namna ya kukusanya hizo fedha kupitia simu zetu za mikononi na nilipendekeza iwe ni hiari.

Leo hii naomba nije na wazo jipya ambalo ni kupendekeza tozo za miamala ya simu zitozwe kwa hiari kama Bima na Bima hiyo itumike kukabiliana na Covid kwani Bima tulizonazo hazitumilki kugharamia matibabu ya covid(gharama ya mitungi, n.k) badala ya tozo hizi kutumika kama chanzo cha kodi kwa serikali jambo linalolalamikiwa na wananchi wengi.

Mfuko huo pia ungetumika kununulia mitungi ya oxygen na vifaa vingine vinavyohusiana na matibabu ya Covid kwa wanachama kama vile gharama za kulazwa, n.k.

Kutokana na tishio la ugonjwa huu na gharama zake kubwa, ninahakika watanzania wengi wangejiunga na hivyo tungeokoa maisha ya watu wengi kupitia Mfuko huu Maalumu wa kupambana na Covid mradi tu serikali isijiingize katika uendeshaji wa Mfuko. Hii ni kwasababu serikali inaweza kuchukua/kujikopesha hela za wanachama na kugharamia miradi yake huku wanachama wakikosa huduma au kuzipata chini ya kiwango.

Watu katika familia mbalimbali wanachangishana na bado wanashindwa kugharamia matibabu ya ndugu zao hasa wale wanaokaa kwenye mitungi ya oxygen kwa muda mrefu.

Tunaangamia law kukosa ubunifu na zaidi kwa kukosa maarifa.
 
Back
Top Bottom