Tozo zinazidi kupalilia mmea uliopandwa kwenye mioyo ya watanzania katika awamu ya 5

Tozo zinazidi kupalilia mmea uliopandwa kwenye mioyo ya watanzania katika awamu ya 5

Nobunaga

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2019
Posts
1,205
Reaction score
5,121
Kati ya nchi nyingi za Afrika, ni nchi chache sana ambazo wananchi wake wake walikuwa na ule uzalendo wa toka moyoni kabisa, ule uzalendo wa kikondoo wa kuambiwa chochote kile na kiongozi hata wa nyumba 10 na ukatekeleza kiroho safi.

Haka ka kitu sijui nikaite ni uzalendo ama ni nini, sijui. Ila nadhani mtakuwa mmejielewa.

Haka ka kitu kaliondolewa(ga) awamu ya 5 ilivyoingia madarakani. Kaliondokaga kabisa sema kilichokuwa kinawa-hold watu ni uoga wa kipindi hiko.

Ilipoingia hii awamu ya 6, watu waliachia pumzi eepphfuuuuu. Hatimaye tulipumua na tukajiona tumerudi kwenye ile status quo ya kipindi cha mzee wa msoga.

Kumbe ni kama ilikuwa mchezo wa doridori. Yani ni kama tulikuwa tunadolishiwa tonge la ugali wakati tuna njaa kalii.

Kwa jinsi uchumi wa dunia ulivyo tight kwa sasa, tulitegemea serikali ingempungumzia mwananchi mzigo kwa kuchukua hatua kadhaa. Lakini toka hii awamu iingie madarakani, ni mwendo wa kumbebesha mwananchi mzigo wa tozo tuu, huku mfumuko wa bei za kila kitu ukiwa juu.

Angalau kipindi cha awamu ya 5 vitu vichache sana ndivyo vilikuwa vinapanda bei, ila sasa kila kitu kimepanda bei, lakini hilo hawalioni ndio kwanza wanazidi kuweka tozo kwenye kila miamala anayoifanya huyu mwananchi mnyonge.

Sasa viongozi kaeni mkijua kuna kitu kilipandwa enzi za awamu ya 5, na sasa awamu ya 6 inakipalilia, nadhani mavuno mtayaona muda si mrefu.

9781409364450.jpg
 
inflation is real lazima tubebe mzigo kwa pamoko ni hivi achomoki mtu, tunaendelea kuset mnyonyo twarudi yakheeee
 
Back
Top Bottom