SoC02 Tozonia, unyongofu wa mfumuko wa bei na dira ya Tanzania

SoC02 Tozonia, unyongofu wa mfumuko wa bei na dira ya Tanzania

Stories of Change - 2022 Competition
Joined
Nov 8, 2016
Posts
23
Reaction score
33
DENI LA TAIFA NA UNYONGOFU WA MFUMUKO WA BEI

Mikopo inatoa uwezo wa kununua baada ya ahadi ya kurejesha, ambapo deni linazaliwa. Uzuri wa deni au ubaya unaamuliwa kwa uzalishaji uliosimamiwa na mkopo huo pamoja na jinsi deni linavyo lipwa.

Mfano: Kukopa fedha kwa ajili ya elimu ambayo mustakabali wake haupo, wanafunzi wakamaliza vyuo wakawa wasio na ajira wala uwezo wa kujiajiri kurudi kwa uwekezaji inakuwa ngumu.

ATHARI ZA DENI NA UNYONGOVU WA MFUMUKO WA BEI

ATHARI ZA MADENI katika nchi zinazo endelea ni UNYONGOFU WA MFUMUKO WA BEI, unyongofu wa mfumuko wa bei ambao madeni mengi yametawaliwa na pesa za kigeni ni ngumu kusimamia kwa sababu watunga sera wanakuwa na uwezo mdogo wa kusambaza maumivu, kwenye kusambaza maumivu ndio unaona athari zake kwenye tozo na kodi.

Katika ripoti ya IMF ya uchambuzi wa uhimilivu wa deni(DSA) inaonyesha hatari ya deni la nje limeongezeka hadi wastani kutokana na athari za janga la korona kwenye mauzo ya nje hali ambayo imedhoofisha uwezo wetu wa kulipa deni la nje.UTALII ndio chanzo kikubwa cha fedha za kigeni kutokuiingia kwa wageni Tanzania kumechangia kusuasua ulipaji wa deni na unaweza pata picha ya kwanini “ROYAL TOUR”. Uwiano wa deni kwa GDP umefikia 41% wakati kizingiti ni 55%. Kuna pengo kati ya mapato ya nchi na matumizi yake.


MAPENDEKEZO

BENKI KUU YA TANZANIA NA UANGALIZI WA USAWA
Mwandishi Ray Dalio anasema Kuna mambo mawili yanayo wakumba watunga sera zetu za fedha ambazo ni kukosa uelewa au kukosa mamlaka ambayo inaweza kusababisha matokeo tofauti kabisa.

Kujilimbikizia madaraka kwenye muhimili mmoja wa serikali kupita kiasi kunaweza kuzidisha mgogoro wa kiuchumi kwasababu inaweza kupunguza kasi ya kufanya maamuzi na kuruhusu wale walio na nia finyu zaidi kuzuia mienendo muhimu ya sera.Tunaona kwamba lengo la msingi la Benki kuu ya Tanzania ni kutunga,kufafanua na kutekeleza sera ya fedha inayoelekezwa kwa lengo la kiuchumi la kudumisha uthibiti wa bei unaowezesha ukuaji wa uwiano na uendelevu wa uchumi wa Taifa.Hili ni kwa mujibu wa sehemu ya 7-(1)(2) ya sheria ya Benki Kuu Ya Tanzania,2006.

Gavana wa Benki kuu kuchaguliwa na Raisi hakumpi yeye mamlaka ya kufanya kazi bila kuingiliwa, Pia deni la taifa linahifadhiwa kwenye mfuko mkuu wa hazina wa serikali kwa mujibu wa Ibara ya 141-(1)(2) ya Katiba ya Jamhuri Ya Tanzania. Ni vizuri watunga sera wakawa ndio wenye nguvu ya kufanya ugawaji wa fedha na kuangalia uwajibikaji na matumizi ya fedha hizi kulingana na sera za fedha na maendeleo ya nchi(kuangalia na usawa, kwa kiingereza check and balance).

RASILIMALI
Marehemu Dr. Reginald Mengi analisema kwenye Kitabu chake kuwa Viongozi wetu wanafanya kazi chini ya dhana kwamba Tanzania ni masikini na hili linapunguza ubunifu na werevu katika kutumia utajiri unao wazunguka kuleta maendeleo ukiangalia rasilimali zetu kubwa na utajiri.

(a) RASILIMALI WATU
Kuna haja kubwa kwa serikali kuwekeza kwa watu, kwa kuhimiza uvumbuzi wa kiteknolojia, kuhamasisha vipaji na ujuzi kwa idadi kubwa ya watu kwasababu ni muhimu kwa ukuaji wa uchumi, hii ni pamoja na kuwa na motisha zinazowahamasisha watu.Wakati serikali ina himiza vijana kujiajiri serikali pia iangalie ni jinsi gani itatengeneza mazingira mazuri ambayo yatawapa motisha ya kujiajiri.

Daron Acemoglu anasema mfanyabiashara ambaye anategemea pato lake kuibiwa, kunyanganywa, au kutozwa ushuru kabisa atakuwa na motisha ndogo ya kufanya kazi.

Mwalimu Nyerere alisema kwenye kitabu chake cha ujamaa kutakuwa na machafuko ya kijamii endapo watu wakigundua kuwa elimu imewatayarisha kwa mustakabali ambao haupo, wahitimu wa chuo walisoma wakitegemea kuajiriwa lakini mazingira ya sasa na hali haviruhusu wahitimu wote kuajiriwa.

Sarafu za kidijitali na ubadilishaji wa fedha ni safu mpya ya kitekinolojia ambapo serikali bado inasita na kuna kiasi kikubwa cha vijana waliojiajiri kupitia safu hii, TANZANIA INAHITAJI FEDHA ZA NJE safu hii ikirasimishwa inaweza kuingizia serikali pesa za kigeni badala ya kupitia mifumo isiyo rasmi pamoja na kupata kodi.

SIASA NA UCHUMI JUMUISHI PAMOJA NA NADHARIA ZISIZOFANYA KAZI
Katika kitabu cha kwanini Taifa linashindwa: chumbuko la madaraka, ustawi na umasikini kinasema uwepo wa taasisi za kisiasa na kiuchumi ambazo hatimaye ni chaguo la jamii zinaweza kushirikisha na kuhimiza ukuaji wa uchumi au zinaweza kuwa za kinyonyaji na kuwa kikwazo cha ukuaji wa uchumi.

Mwanauchumi mashuhuri anasema “Nchi maskini ni maskini si kwa sababu ya kijiografia au utamaduni wao, au kwasababu viongozi wao hawajui ni sera gani zitawatajirisha raia wao”.inaendelea kuwa sera zinachaguliwa si kwasababu ni uchumi mzuri au njia bora ya kuendeleza nchi, sera zinachaguliwa kwasababu ni siasa nzuri.

Katika nchi zinazo endelea wanasiasa wamekuwa wakitumia nadharia zisizofanya kazi kufanya maamuzi. IKIWA KIWANGO CHA MAPATO HAKIKUI LAKINI KODI NA MFUMUKO WA BEI UNAONGEZEKA KWA KASI, HILI LINASAIDIA VIPI MAENDELEO?

MFANO: Kodi ya zuio(withholding tax) kwa wapangaji wa nyumba binafsi ni changamoto kwa mpangaji na mwenye nyumba, na swali la kimantiki kujiuliza ni kuwa mtu anayetegemea kupata 10,000?= kwa mwezi na sasa anapata 9000/= ni kipi kinamzuia yeye kupandisha kodi ili aweze kuendelea kupata 10,000/=, na endapo hili ni sahihi ni nani mwathirika wa hili kama sio mpangaji?.

Changamoto kubwa inayojitokeza ni kwa mpangaji wa nyumba binafsi pamoja na mpangishaji wa nyumba binafsi ni kuwa wanakatwa kodi kwa kipato ambacho hakijaongezeka, Makini Mpangaji wa nyumba binafsi yuko hatarini kuongezewa kodi kwa kipato kile kile wakati mpangishaji wa nyumba binafsi anakatwa kodi kwa pato lile lile hivyo ni lazima kwake kutafuta njia ya kuongeza hicho kipato.SWALI LA MSINGI KWA VIONGOZI DHANA HII INAFANYA KAZI VIPI KULETA MAENDELEO KWA KUHAKIKISHA MTU BINAFSI ANAPATA MAENDELEO NA KUISAIDIA NCHI YAKE KUENDELEA.

“Inawezekana bei tunayouzia data ni ya chini ukienda nchi kama Africa kusini, Uingereza, Canada kwa sababu uchumi wao ni mkubwa, sisi bado watu wetu ni masikini na ndio maana kama serikali tunachofanya ni kudhibiti tusipande sana”. Hii ni siasa nzuri lakini inasaidia vipi pato la mtu kuongezeka?

Kwa sababu bado tunaona mabadiliko ya vifurushi jinsi siku zinavyo zidi kwenda pamoja na tozo zikipambania kipato kile kile na sasa nadhani tunaelewa kwanini aina hii ya mawazo inapunguza ubunifu na werevu katika kutumia utajiri unaopatikana kutuzunguka kufanya maendeleo kama marehemu Dr. Reginald Mengi alivyohusia apo mwanzo.

Tunahitaji uchumi na siasa jumuishi pamoja na SERA zinazofanya kazi.

MWISHO

0712775734
tanzania-external-debt-stock-2022-08-25-macrotrends.png

Chanzo cha picha google(macrotrend).
 
Upvote 1
Back
Top Bottom