TP Mazembe yafanya mauaji ya kinyama Klabu Bingwa Afrika: Yaitundika Club Africain goli 8 bila huruma

ngogo s ngogo

Senior Member
Joined
Nov 29, 2015
Posts
134
Reaction score
81
Habari wanajamvi, natumai mu wazma kbsa.
Leo tarehe 2/2/2019. Kuna michezo sita kutoka ktk makundi yote manne yaani A, B, C na D.

Katika Group A. Timu ya Lobi Star ya Nigeria ikiwa nyumbani imekubali kichapo cha bao moja kwa sifuri (0 - 1) kutoka kwa timu ya Waydad Athletic Club kutoka nchini Morocco.

Group B. Timu ya Fc Platinum ya Zimbabwe nayo imefungwa nyumbani (0 - 1) bao moja kwa sifuri na timu ya Horoya kutoka nchini Guinea.

Mchezo mwingine wa Group B. Ni hapo saa 4:00 usiku Kati ya wenyeji Orlando Pirates ya Afrika kusini dhidi ya mabingwa watetezi timu ya Esperance -Tunis kutoka nchini Tunisia.

Group C. Timu ya TP MAZEMBE ya DRC ikiwa nyumbani Lubumbashi imepata ushindi mnono wa magoli 8 - 0 dhidi ya timu ya Club Africain kutoka nchini Tunisia. KWELI HAYA MASHINDANO NI MAGUMU

Group D. Mechi mbili kutoka kundi hili zinatarajiwa kupigwa hapo baadae.

Saa 7:00 Jion, Timu ya As Vita Club ya DRC itakuwa ktk uwanja wake kuwaalika timu ya Js Saoura kutoka nchini Algeria.

Baadae kwenye mida ya saa 4:00 Usiku, Mabingwa wa kihistoria nchini Misri na Africa kwa ujumla timu ya Al Ahly wataikaribisha timu ya SIMBA YA TANZANIA.

My take.
Ktk haya mashindano hakuna cha ugenini wala nyumbani, ukizembea unafungwa popote.

KARIBUNI

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duh,wakongo ni mbogo,nilidhani record ya goli 5 kwa simba isingevunjwa kwa hatua hii.
 
Duh,wakongo ni mbogo,nilidhani record ya goli 5 kwa simba isingevunjwa kwa hatua hii.
 
tusubiri mechi ya Leo ndio tukomenti...
 
Naomba simba aingie atua ya 16 apangwe na mazembe tuje tushudie kiama kingine mtu analambishwa mchanga kama wote.
 
Huu uzi umekuja kwa kuwepo na game ya Simba hapo baadae,,btw Simba anakufa leo,kuanzia gori 4 na kuendelea znamhusu[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Naomba simba aingie atua ya 16 apangwe na mazembe tuje tushudie kiama kingine mtu analambishwa mchanga kama wote.
Hatua ya 16? Au masikio yangu nimesikia vbay

[emoji375][emoji375]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…