TPA kuanza kuendesha eneo la TICTS Januari 2023

TPA kuanza kuendesha eneo la TICTS Januari 2023

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), imesema kuanzia Januari Mosi, 2023 mamlaka hiyo italiendesha eneo lililokuwa likitumiwa na Kampuni Binafsi ya Kimataifa ya Kuhudumia Makontena Tanzania (TICTS).

Kauli hiyo, imetolewa leo Jumatano Desemba 21, 2022 na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Juma Kijavala wakati akifungua semina ya kuwajengea uwezo wanahabari kuhusu utendaji kazi wa mamlaka hiyo.

Hatua hiyo imekuja baada ya mkataba wa kati TPA kufikia ukomo Septemba 30 mwaka huu, licha ya kuwepo kwa kipengele cha kuuhisha lakini menejimenti ya mamlaka hiyo imekataa. TICTS imehudumu katika Bandari ya Dar es Salaam kwa miaka 22 sasa, tangu iliposaini kutoa huduma ya makontena na mizigo mingine kazi ambayo itafanywa pia TPA.

Katika maelezo ya Kijavala, alianza kwa kueleza kuwa sio kwamba mkataba kati ya TPA na Ticts umevunjwa bali umekwisha muda wake, kwa hiyo mamlaka hiyo inachukua eneo hilo na kuliendesha kuanzia Januari Mosi mwakani.

"Kama Serikali itaamua kumpa mwekezaji mwingine sawa au itaamua eneo lile kuendeshwa na TPA sawa, lakini tunawahakikishia huduma zitakuwa bora zaidi ya hapo. "Unapokuwa umepangisha nyumba yako, mkataba wa mpangaji wako ukiisha una hiyari kumuongezea au kutomwongezea si ndio? Mkataba wa Ticts umekwisha," amesema Kijavala.

Kijavala amesema wafanyakazi wote wa TICTS ajira zao zipo salama wataendelea kutelekeleza majukumu yao upande wa makontena na watalipwa stahiki zao kama ilivyokuwa awali na TPA. "Ajira zitakuwa salama na kuanzia Januari Mosi huduma zitaboreshwa kuliko ilivyokuwa," amesema Kijavala.

MWANANCHI
 
Efficiency ikiongezeka hapatakuwa na tatizo.
Shida ni wakizidiwa mizigo
 
Binafsi siamini katika serikali kuendesha jambo likafanikiwa zaidi ya sekta binafsi!
 
Pia, baada ya makataba kuisha, je TPA imenunua mitambo ya TICTS? Kwa TSH ngapi?
 
Back
Top Bottom