TPA yatakiwa kukusanya mapato yatokanayo na wharfage kama ilivyo sehemu zote duniani

Pfizer

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2021
Posts
590
Reaction score
807
WADAU wa Bandari wameishauri serikali kuruhusu Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kuendelea kukusanya tozo itokanayo na huduma za bandari (wharfage) kama ilivyo sehemu zote duniani.

Ushauri huo umetolewa wiki hii na wadau hao pamoja na wachumi, ikiwa ni miezi michache baada ya wabunge kutoa ushauri huo kwa serikali.

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inakusanya zaidi ya Sh Trilioni moja kwa mwezi nje ya wharfage ambayo ni shilingi bilioni moja kwa mwezi.

Taarifa zinaeleza TRA wanang’ang’ania wharfage wakidai ni muhimu kwao bila kujali ufanisi wa bandari utaongezeka mara dufu mapato yatokanayo na kodi.

Ushauri huo umekuja wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt Samia Suluhu Hassan, ameonyesha kuridhishwa na mafanikio iliyoyapata TPA hadi kuongoza katika taasisi zilizotoa gawio serikalini kwa kutoa Shilingi bilioni 153 9

Mtaalamu wa masuala ya bandari nchini, Bw Emmanuel Mallya, amesema kwa serikali kutoruhusu TPA kukusanya wharfage ni sawa na kuizuia kukua na kukwamisha ongezeko la ufanisi unaoletwa na uwekezaji toka sekta binafsi.

“TRA ni kama vile wanataka kuiziba pumzi bandari, maana 'wharfage' siyo kodi bali ni tozo inayotozwa kwa huduma za bandari kusaidia kuboresha miundombinu iwe endelevu,” anasema Bw Mallya.

Be Mallya ambaye ni Mwenyekiri wa Bodi ya Wadhamini wa Chama cha Mawakala wa Meli Tanzania (TASAA), anasema ni vyema Mamlaka ya Mapato Tanzania ikaendelea na majukumu yake ya kukusanya kodi ambayo sehemu kubwa inatokana na ufanisi wa huduma za bandari.

“Sasa kama unataka ukusanye kodi zaidi, lazima uiache bandari iwe na uwezo wa kujiendesha na kuboresha miundombinu na huduma nyingine nyeti zilizo ndani ya mamlaka,” anasema.

Wakichangia bajeti ya Wizara ya Uchukuzi hivi karibuni, Wabunge walisema ili TRA iweze kukusanya kodi zaidi, inabidi TPA iachwe ikusanye 'wharfage' kwa ajili ya kuboresha miundombinu, huduma na usalama bandarini.

Mbunge wa Viti Maalumu, Esther Maleko, pamoja na kazi nzuri inayonywa na TPA chini ya Mkurugenzi wake Mkuu, Plasduce Mbossa, serikali iiruhusu mamlaka hiyo kukusanya 'wharfage'.

Zacharia Elie, mchumi na mfanyabiashara wa magari anasema endapo TRA itakusanya 'wharfage' itarudisha nyuma uwezo wa TPA ambayo kimsingi inafanya vizuri.

"TPA imeonyesha uwezo mkubwa wa kujisimamia na kama itaachiwa 'wharfage' itakuwa na uwezo mkubwa wakufanya makubwa,"alisema.

Akiwa Bungeni Waziri wa fedha, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (mb), wakati akiwasilisha bungeni mapendekezo
Ya Serikali kuhusu makadirio ya
Mapato na matumizi kwa Mwaka 2024/25 Tarehe 13 juni 2024 Jijini Dodoma amesema:

" Mheshimiwa Spika, napendekeza kufanya marekebisho kwenye Sheria ya Bandari ya mwaka 2004 ili kurejesha jukumu la kukusanya tozo ya matumizi ya miundombinu ya bandari (wharfage) kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA).

Aidha, mapato yatakayotokana na tozo hizo yatawekwa katika akaunti maalum ya TPA iliyopo Benki Kuu ya Tanzania na matumizi yake yatafanyika baada ya kuomba na kupata idhini ya Mlipaji Mkuu wa Serikali.[/I]

Lengo la hatua hii ni kuiwezesha Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania kupata fedha kwa wakati kwa ajili ya maboresho ya miundombinu ya Bandari na hivyo kuongeza ufanisi wake."

====

Pia soma: LIVE - Hotuba ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025, leo Juni 13, 2024 Bungeni, Dodoma
 
View attachment 3016515

====

Pia soma: LIVE - Hotuba ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025, leo Juni 13, 2024 Bungeni, Dodoma
Ni kweli kabisa, haingii akilini TRA wanakusanyaje na kung'ang'ania mapato yasiyo ya kwao? Wizi Mtupu kudadeki
 
Back
Top Bottom