Pfizer
JF-Expert Member
- Mar 25, 2021
- 590
- 807
UFAFANUZI KUHUSU TOZO YA WHARFAGE
JUMAPILI MACHI 10, 2024
DAR ES SALAAM
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandnari Tanzania (TPA) inapenda kutoa ufafanuzi kuhusu tozo ya Wharfage kwa Wateja na Wadau wa huduma za Bandari na kuweka usahihi wa taarifa kwa Umma kwa ujumla kama ifuatavyo.
Wharfage ni tozo ya Bandari ambayo inatozwa kulingana na mahali mzigo unakokwenda. Kwa mizigo ya ndani ya nchi, tozo hii inatozwa kwa thamani ya mzigo (Custom Value) ambayo kiwango chake ni 1.6% kwa mzigo wa kasha pamoja na mzigo usiokuwa katika kasha (Loose Cargo)
Kwa shehena za nje ya nchi (Transit) inatozwa:-
a) Kwa mizigo isiyokuwa katika kasha (Loose Cargo) inatozwa kwa uzito au ujazo kwa kiwango cha Dola 3 za Kimarekani.
(b) Kwa mzigo wa kasha inatozwa kwa Dola 90 kwa kasha la futi 20 na Dola 180 kwa kasha la futi 40.
2. Kwa kutumia hoja ya Mteja aliyesambaza malalamiko yake katika mitandao ya kijamii mwishoni mwa Wiki hii, ni dhairi kwamba shehena anayoizungumzia itakuwa ni ya ndani (Domestic/Local cargo) ambayo ndiyo inatozwa kwa thamani.
3. Kwa thamani ya 42,855,357.51 wharfage bila VAT itakuwa 685,685.72 (1.6% γα 42,855,357.51) ukiweka na VAT 18%. Kwa hiyo, kiasi kitakacholipwa ni 809,109.15 na si 1,759,768 kama inavyodaiwa.
4. Kwa kuwa tozo hizi zinatozwa kwa mfumo bila kuingiliwa na watu (No human intervation), hakuna uwezekano wa kukosea kwa maana ya kumtoza mteja zaidi au pungufu ya kiasi kinachotakiwa kulingana na thamani ya mzigo wake. Hata hivyo kama kuna mteja ana malalamiko tunawaomba kufika kuwasilisha malalamiko hayo kwenye ofisi ya Mkurugenzi wa Bandari ili lipatiwe ufumbuzi wa haraka.
5. Ifahamike kwamba hadi sasa Bandari ya Dar es Salaam bado inaendeshwa na TPA, DPW bado hajaanza kazi, na DPW atakapoanza Umma utajulishwa.
6. TPA inapenda kuujulisha Umma kwamba, hata DPW itakapoanza kuendesha Bandari ya Dar es Salaam, tozo ya Wharfage itaendelea kuwa mapato ya TPA na si DPW kwa mujibu wa makubaliano kati ya TPA na DPW na kwamba kwa sasa Wharfage inakusanywa kwa mfumo wa TANCIS ambao uko chini ya TRA na itaendelea kuwa hivyo hata baada ya DPW kuanza uendeshaji wa bandari ya Dar es Salaam.