TPBRC kupelekana mahakamani, wadau wamtaka Sir Joe anea kurudi madarakani

TPBRC kupelekana mahakamani, wadau wamtaka Sir Joe anea kurudi madarakani

Linguistic

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2021
Posts
3,669
Reaction score
8,268
Anaandika Mdau Wa Ngumi Za Kulipwa Jay Msangi
.
Wacha inyeshe tuone panapovuja ila kiukweli huu uchaguzi wacha ufanyike ila batili na watu wakitaka kuupinga mahakamani unaweza ukafutwa kabisa

Sababu za kuupinga uchaguZi kuwa ni batili ni hizi :

Uchaguzi unaotaka kufanywa ni uchaguzi kujaza nafasi ya raisi wa shirikisho la ngumi za kulipwa tanzania ambayo iliachwa wazi baada ya aliyekuwa anashikilia nafasi hiyo sir joe anea kuandika barua ya kuomba kujiuzulu

Joe anea aliandika barua ya kuomba kujiuzulu kwa sababu za kiafya kama tulivyosikia kwenye vyombo vya habari

Barua ya joe anea ya kujiuzulu ilitakiwa iletwe kwenyr mkutano mkuu wa wadau/ wanachama na kujadiliwa na mkutano mkuu ndio utakaotoa maaumuzi kama umeridhia sir joe anea ajiuzullu hivyo ndivyo katiba ya tpbrc inavyotaka

Kwa sababu mkutano mkuu haujaitwa nawadau / wanachama hawajapitisha / hawajajibu hiyo barua ya sir joe kujiuzulu basi katiba ya tpbrc bado inamtambua bwana joe anea kuwa ni raisi

Si TPBRC wala bmt hawana mamlaka ya kukiuka katiba bila maridhiano ya mkutano mkuu sasa ni nani alikubali maombi ya sir joe anea kujiuzulu. Mtambue hiyo barua tunayoambiwa sir joe anea ameiandika hakuna mdau/ mwanachama yeyote aliyeiona ila pia tukumbuke barua hiyo ilikuwa ni maombi ambayo mkutano mkuu pekee ndio unaoweza kutoa maamuzi

Tusitengeneze bomu na baadaye watu wakarudi mahakamani kuomba mahakama itutafsirie sheria / katiba yetu tuliyoiandika wenyewe ili ituongoze

Sulusheni: Joe anea arudi kwenye kiti chake au waitishe mkutano mkuu tuijadili barua yake ya kujiuzulu. Katiba bado inamtambua joe anea bado ni rais wa shirikisho la ngumi za kulipwa tanzania na aga peter bado ni makamu wake

Tusiseme tulikuwa hatulijui hili watu wanajipanga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom