TPBRC: Mandonga hajafungiwa kupigana

TPBRC: Mandonga hajafungiwa kupigana

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
1692097361431.png
Rais wa Kamisheni inayosimamia ngumi za kulipwa Tanzania (TPBRC) Chaulembo Palasa amesema Bondia Mtanzania Karim Mandonga hajafungiwa kama inavyoripotiwa na baadhi ya Vyombo vya Habari bali sheria za ngumi nchini zinamtaka Bondia yoyote atayepoteza pambano kwa KO au TKO kabla ya kurudi ulingoni kwa pambano jingine kupimwa afya.

Palasa mesema kwakuwa Mandonga alipoteza dhidi ya Moses Golola Raia wa Uganda July 29 2023 Jijini Mwanza kwa TKO haruhusiwi kupanda ulingoni kucheza pambano jingine hadi afanyiwe vipimo vya afya kwa usalama wake.

Hivyo Mandonga jana amefanyiwa vipimo vya afya (MRI ya kichwa) katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na majibu yatatoka leo August 15, 2023 saa 9:00 Alasiri kama yupo sawa kiafya kurejea ulingoni kwani ana pambano Zanzibar August 27,2023.
 
Wamuache tu afie ulingoni kwani ndiyo matamanio ya washabiki wake
 
Back
Top Bottom