Asante Sana, nilikua najiuliza kwanini serikali haichimbi visima vyake?!
Sasa naona busara zimetumika.
Angalizo,
Nilidhani dhamira hii ingepelekwa bungeni, ili Bunge li ridhie uchimbaji huu wa gesi kupitia serikali.
Uchimbaji wa gesi ni Kama mchezo wa kamari, ukiliwa unaridhika aukipata ni bonge la bingo.
Hivo ijulikane hizo billion 200 zinaweza potea pale ambapo gesi itakapofikiwa ikiwa ni kidogo kiasi kwamba haiwezi ku sustain operations. Nahivo kuhitajika billion nyingine kadhaa za kufukia na kuondoa mitambo kwenye shimo
Yes! hasara hasaa!
.
Na hapo ndo panatofauti na kamari, kamari ukiliwa unaliwa ile ulio weka, Kwa gesi ukiliwa inabidi ufukie na shimo Kwa gharama zaidi.
Kwanini Bunge lishirikishwe?! Sababu tukiliwa, tuliwe Kama nchi, tusije shikana mashati na baadhi ya watu kuonewa kisiasa.
Hata hivo nappngeza jitihada hizi na tuliombee taifa letu na tufanikiwe kwenye hili.
Hongera Sana walileta na watakaotekeleza Jambo hili.