TPL: Simba SC vs African Lyon - October 6, 2018

sembo

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
4,350
Reaction score
3,451
Baada ya 'kuwakosa kosa' Yanga SC, Bingwa mtetezi wa TPL, Simba SC leo anarejea dimbani tena kupambana na African Lyon katika muendelezo wa TPL.
Mechi hii itachezwa katika dimba la Taifa, kuanzia saa 1 kamili usiku.

Update 1.
Jeshi La Maangamizo la Simba SC
Kikosi Cha Kwanza
1. Aishi Manula
2. Shomari Kapombe
3. Mohammed Hussein
4. Erasto Nyoni
5. Pascal Wawa
6. James Kotei
7. Jonas Mkude
8. Mo Ibrahim
9. Meddie Kagere
10. Emmanuel Okwi
11. Clatous Chama
Kikosi Cha Akiba
1. Deogratius Munishi
2. Juuko Murshid
3. Nicholas Gyan
4. Said Ndemla
5. Shiza Kichuya
6. Adam Salamba
7. Haruna Niyonzima

FT: Simba SC 2-1 African Lyon
 
Kwa upande wa Simba SC..

1. Aishi Manula, Shomari Kapombe, John Bocco na Jonas Mkude waliokuwa wameitwa kambini Stars kwa ajili ya kujifua kujiandaa na mchezo wa kufuzu kuelekea AFCON 2019 dhidi ya Cape Verde wamerejea.
2. John Bocco ataendelea kukosekana katika mechi ya leo, akiwa andelea kutumia adhabu ya kadi nyekundu aliyopewa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Leo mafundi wa mpira kuwahi kushudiwa katika miaka ya hivi karibuni, Juuko Murshid na Haruna Niyonzima wamerejea katika kikosi cha Mnyama mkali mwituni, Simba SC.
Wanaanzia katika kikosi cha akiba.
 
Kutoka kwa Governor, De Le Boss, Haji Manara..
Tuna sababu nyingi sana za kupata Matokeo chanya kwenye mchezo wetu wa leo dhidi ya African Lyon leo Saa Moja Usiku pale Taifa..na tunajua jinsi tulivyojiandaa na kwa matakwa yake Mola,Inshallah tutashinda...
Viingilio ni 15,000,10,000 na 5,000..

Wapenda soka la kasi, mipasi ya kutosha, magoli ya videoni, maudambwi udambwi.. karibuni Taifa
 
Leo mafundi wa mpira kuwahi kushudiwa katika miaka ya hivi karibuni, Juuko Murshid na Haruna Niyonzima wamerejea katika kikosi cha Mnyama mkali mwituni, Simba SC.
Wanaanzia katika kikosi cha akiba.
Hivi nyie mbumbumbu kwa nini mmeua kipaji cha Haruna? Kila le heri African Lyon, nyie ni simba wa Afrika hamuwezi mshindwa simba wa bunju!
 
Nimapata taarifa kua ... Ile kazi ya kukusanya vijiji vya ujamaa na kutengeneza mji aliyoinza Chama wiki iliyopita itaendelea leo na zoezi hilo limefikia patamu.
Karibuni Taifa leo mshuhudie muendelezo wa hiyo kazi.
 
Kichuya kuanzia benchi ni sawasawa kabisa.
Okwi pia angeanzia benchi.
Leo ilikuwa zamu ya akina, Niyonzima, Juuko, Salamba, Gyan, kuanza.
 
Point 3 tu ndio muhimu kwetu Simba.
kila la kheri
 
Kichuya kuanzia benchi ni sawasawa kabisa.
Okwi pia angeanzia benchi.
Leo ilikuwa zamu ya akina, Niyonzima, Juuko, Salamba, Gyan, kuanza.
Gyan licha ya kumudu nafasi ya beki lakini ni Striker yule.Naunga mkono hoja kwamba bwana Emanuel Okwi angempusha ili nae ajaribu bahati yake mana Mechi iliyopita alizingua sana.Kichuya amedrop sana kiwango.Maybe Kuleewa sifa,Starehe au Upepo kama wa mshambuliaji mmisri Mo Salah.Kila laheri chama langu Simba likiongozwa na Chama kwenye kiungo
 
Simba ni Taifa Kubwa. Mchezaji wa kiwango kwenu Mbute FC, kwa Simba ni kawaida sana kama wengine tu

Ndo maana mchezaji anayekaa benchi Simba, akienda Mbute anakuwa star kikosi cha kwanza..Kama Ajibu, This Is Simba
Hivi nyie mbumbumbu kwa nini mmeua kipaji cha Haruna? Kila le heri African Lyon, nyie ni simba wa Afrika hamuwezi mshindwa simba wa bunju!
 
Kuna maandishi yanapita pale chini Azam sport 2 "Kocha msaidizi Simba Masoud Juma akalia kuti kavu Simba".
Wasije wakatuharibia tu timu yetu,inaonekana washapanga kumfukuza Masoud
 
Kuna maandishi yanapita pale chini Azam sport 2 "Kocha msaidizi Simba Masoud Juma akalia kuti kavu Simba".
Wasije wakatuharibia tu timu yetu,inaonekana washapanga kumfukuza Masoud
Wamesema wanamfukuza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…