sembo
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 4,350
- 3,451
Hatimaye 30/09/2018 imefika. Leo ni siku ambayo ilikua ikisubiriwa kwa hamu sana ambapo, Bingwa Mtetezi wa TPL, Simba SC atamkaribisha Yanga SC katika dimba la Taifa Stadium.
Mechi hii inatarajiwa kuanza mnamo saa 11 kamili.
Update 1.
Jeshi La Maangamizo la Simba SC
Kikosi Cha Kwanza
1. Aishi Manila
2. Shomari Kapombe
3. Mohammed Hussein
4. Erasto Nyoni
5. Pascal Wawa
6. James Kotei
7. Jonas Mkude
8. Clatous Chama
9. Meddie Kagere
10. Emmanuel Okwi
11. Shiza Kichuya
Kikosi Cha Akiba
1. Deogratius Munishi
2. Paul Bukaba
3. Asante Kwasi
4. Said Ndemla
5. Mo Ibrahim
6. Adam Salamba
Update 2.
Kikos cha Yanga SC
1. Benno Kakolanya
2. Paul Godfrey
3. Gadiel Michael
4. Vicent Andrew 'Dante'
5. Kelvin Yondani (C)
6. Feisal Salum 'Fei toto'
7. Deus Kaseke
8. Papy Tshishimbi
9. Herietier Makambo
10. Ibrahim Ajibu
11. Mrisho Ngasa
SCORE UPDATES:
Hadi mapumziko (HT): Simba 0-0 Yanga (Kipindi cha kwanza kimetawaliwa zaidi na Simba)
SCORE UPDATES:
FT: Mpira umeisha.. Simba SC 0-0 Yanga SC
Watani wa Jadi, Wekundu wa Msimbazi Simba SC na Yanga Africans leo wametoshana nguvu ndani ya dimba la uwanja wa Taifa baada ya kutoka suluhu ya bila kufungana ikiwa ni muendelezo wa michezo ya Ligi Kuu Soka Tanzania Bara.
Simba ambayo ni mabingwa watetezi wa kombe hilo walionekana kumiliki mpira kwa muda wote wa mchezo huku washambuliaji wake wakiongozwa na Meddie Kagere wakikosa umakini katika kumalizia nafasi ambazo walizipata.
Katika mchezo huo Simba ilifanikiwa kupata kona 10 huku Yanga wakipata kona moja lakini safu nzuri ya Yanga chini ya Nahodha, Kevin Yondani iliweza kusimama imara ingawa kipa wa mabingwa hao wa Kihistoria, Benno Kakolanya anapaswa ashukuriwe kwa kuokoa idadi kubwa ya mashuti yaliyoelekezwa langoni mwake.
Huu umekua ni mchezo wa kwanza pia kwa makocha wa timu zote mbili, Patrick Aussems wa Simba raia wa Ubelgiji na Mwinyi Zahera wa Yanga ambaye ni Mkongo.
Kwa matokeo hayo, Yanga inafikisha alama 13 na kukwea hadi nafasi ya pili sawa na Mtibwa Sugar, huku Yanga ikisalia nafasi hiyo kutokana na uwiano mzuri wa magoli ya kufungwa na kufunga.
Simba inaongeza alama moja na kufikia alama 11 na kukwea hadi nafasi ya nne ya msimamo wa ligi kuu huku Mbao Fc ya Mwanza ikiendelea kusalia kileleni mwa msimamo wa ligi kwa alama zake 14.