TPLB yasema haitatoa leseni kwa vilabu vitakavyokuwa vinadaiwa msimu ujao

TPLB yasema haitatoa leseni kwa vilabu vitakavyokuwa vinadaiwa msimu ujao

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Bodi ya ligi kuu Tanzania bara (TPLB), imesema haitatoa leseni kwa klabu yoyote msimu ujao, ambayo itakuwa inadaiwa na wachezaji, makocha na hata taasisi mbalimbali.

Tamko hilo limetolewa na mwenyekiti wa bodi hiyo, Steven Mguto leo Juni 15, 2020, ambaye amesema kumekuwa na changamoto ya vilabu vingi nchini kulimbikiza madeni na kutolipa stahiki za wachezaji kwa wakati tofauti na makubaliano.

Mguto amewatoa hofu wachezaji ambao wamemaliza mikataba na vilabu vyao, lakini wameagizwa kuendelea kuvitumikia kwa makubaliano hadi Julai 31, kutokana na ligi kuchelewa kumalizika kutokana na janga la Covid 19.

Vilabu vya Tanzania vikiwemo Simba na Yanga vimekuwa vikilalamikiwa na baadhi vya wachezaji ambao hata wakiachana nao, hawalipwi pesa za usajili na hata mishahara, lakini wamekua hawapati haki kwa kuwa hakuna adhabu zinazochukuliwa.

Chanzo: EATV
 
Back
Top Bottom