Viongozi na Wazalendo;
Nimewasoma. Mafikirio yalikuuwa huenda huko nyuma mmekuwa mkipitia mabandiko yote ya TPN. Nadhani nimekosea si wote wanafanya hivyo ingawa kwa hakika najua kuwa maswali haya yameulizwa mara nyingi sana na yamejibiwa kwa kiwango cha kuridhisha.
Tuanze upya:
1.Ningependa kujua mpaka sasa mmefanya kitu gani kusaidia Taifa
Links ambazo maswali yanayofanana na hayo yaliulizwa na pia tazama report iliyoambatanishwa:
https://www.jamiiforums.com/matanga...-karibuni-tanzania-professionals-network.html
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...nzanians-diaspora-summit-december-2009-a.html
https://www.jamiiforums.com/habari-hoja-mchanganyiko/16002-tuzo-kwa-mtanzania-aliyefanya-vyema.html
Katika ICT: Hatujafanya mengi sana kwani TPN imeanza Mwishoni mwa Mwaka 2007. Hata hivyo kuna machache yaliyofanywa:
- Kupitia baadhi ya members wake, tumeshiriki katika kuandaa mkakati wa Mkonga "Optic Fiber" ya ndani ya nchi ambayo muda si mrefu.
- Maandalizi ya report ya mkakati wa utekelezaji wa Bill Gate/JK MoU ya kusaidia ICT katika area ya Elimu, Tourism na E-Government.
- Na sasa tunashirikiana kwa karibu na COSTECH kuandaa mkakati ni vipi Science na Technology vitasaidia kuondoa umasikini. Katika hili DG wa COSTECH atakuwepo katika hafla pia kuongelea ni wapi tumefikia na nini tutafanya pamoja.
2.Ningependa kujua mtazungumzia nini huku katika hiyo hoteli
- Maandalizi ya Diaspora Summit December 2009. Angalia Link hapo juu.
- Maandalizi ya Tuzo ya Mtanzania aliyefanya vema. Angalia Link hapo juu.
- Wazo la mkakati wa kutunisha mfuko kupitia Carnival Festivals za Tamaduni za kitanzania ili kuanzisha VIJIJI VYA KIJASILIAMALI na INCUBATORS CENTRES.
- Networking kwa ajili ya Ujuzi, Mitaji na Masoko.
3.Nani atatoa maada na siyo suala la kusema kutakuwa na Mziki na get together(lengo lenu na imekuwa tabia ya watanzania wengi)...Suala la msingi mnalotakiwa kufanya ni kujadili mambo muhimu yahusuyo Taifa letu na hata ikiwezekana mjadili kwa siku nzima bila kuwapo matukio mengine yasiyo ya muhimu.
TPN katika mwaka huwa tuna Networking Events zenye watoa maada walau mara moja kwa miezi miwili. Pia tunashirikiana na British Council ambapo kila mwezi kuna maada mbalimbali.
Katika event ya sasa nia ni kujumuika na kutumia muda mwingi watu wafahamiane zaidi na kunetwork. Hata hivyo kutakuwa na waongeaji (Very Briefly)wafuatao:
- DG wa COSTECH
- Director wa UDEC ambao mwaka huu TPN imeshirikiana nao kufanikisha mashindano ya BUSINESS PLAN iliyoshirikisha wajasiliamali zaidi ya 350 na ambao tunaweka mikakati ya kuinuana.
-MATRON wa TPN
-Mwakilishi wa TPN
- Kutakuwa pia na Interraction
Inavyoonessa hiyo ni deal vtu na vielelezo vya kuwa kuna vyumba ya double na single inaonesha mnataka watu wakapumzike tu huko na nyie mfaidike.
Hakuna mtu anayekuzuia kufikiria utakavyo. Wewe ni kiumbe huru.
Sanctus nakufahamu sana kwa muda mrefu hata kabla haujaja nchini,kwa kusoma baadhi ya vitu ulivyoandika na hata kwa kusikia na kukuona ukiongea. Binafsi kukuona kwako na wewe kuwa na shahada yako ya kwanza ambayo siyo ya mambo ya IT wala ICT,Nakuona kama optunist mwwenye lengo binafsi(kama Wahindi).
Nashukuru kama unanifahamu. Kama nilivyosema siwezi kukuzuia kufikiri utakacho. Ni kweli kuwa sina shaada ya kwanza ya ICT na kama unanijua utagundua kuwa mpaka namalizi shahada yangu hakukuwa na course za ICT zaidi ya Options katika Faculties mbalimbali. Kwa kuwa unanifahamu, bila shaka unajua shahada yangu ya kwanza na ya pili nilisoma nini na wapi.
Opportunisti mwenye Malengo Binafsi - hilo nakuachia wewe ufikiri utakavyo. Hata hivyo records zangu na wale ambao nimefanya nao mambo mbalimbali, zinapingana kabisa na wazo lako.
Nachoana ni kuwa ,Kungekuwa na chombo muhimu chenye wataalam wa ICT hapa Tanzania,Hata vitu kama Vitambulisho vya kitaifa vingeanzia hapa.Ila TNP imejaa watu wale wale ambao wamekuwa wakiipeleke serikali yetu katika gharama kubwa zisizo na msingi (nyingi za kifisadi).
TPN na wala si TNP kama unavyoiita na Mtandao wenye madhumuni makubwa wa kuwafanya wanataaluma washirikiane na kubuni mikakati ya kuwezeshana kiuchumi. Unaweza ukapitia hapa:
TPN - Homepage
Nijuavyo kuna vyama mbalimbali vya kitaaluma na hata cha ICT kipo na kina viongozi wake. Kwa maoni yangu vyama visivyo vya kiserikali NGO vinaweza tu kuishauri serikali au kuweka pressure.
Kama una ushahidi kuwa TPN imekuwa ikiipelekea serikali katika gharama kubwa, si vibaya ukitoa ufafanuzi ili tuamini unachoandika. Nijuavyo mimi, mengi unayoongea kuhusu TPN ni kinyume cha tunayoyafanya na kupanga kuyafanya.
Kuna watu kama kina sawe ambao wamekuwapo pale UTUMISHI kwa muda mrefu ial hakuna chochote ambacho wanweza kujisifia.
Siwezi kumjibia Sawe. Ila najua kuna mazuri mengi aliyoyafanya pia. Just for interest Mzalendo Gembe: Ni nini ambacho umeifanyia Nchi ambacho wewe binafsi unaweza kujisifia na TPN ijifunze kutoka kwako?
TNP ni kama kijiwe cha kisiasa ambacho kimekosa mwelekeo.
TPN kama inayojitambulisha, haina mlengo wa Kisiasa, Kidini, Kijinsia, rangi wala mwegemeo wa namna yoyote. TPN si Kijiwe ni mtandao unaohusisha watanzania walioko ndani na nje ya nchi. Na ndiyo maana pia tunaandaa Diaspora Summit.
Tunahitaji umoja wa kaifa katika kumaliza matatizo yanayotukabili katika njanja zote.Kuanzia siasa hadi huku kwewnye ICT.
Nashukuru kama umeliona hilo. Hicho na mengine ndiyo TPN inajaribu kufanya. Tuungane mkono itapendeza zaidi. Kama kunamapungufu, tusaidiane na kusahihishana. Nadhani hiyo ndiyo njia sahihi ya kuendelea mbele. Kama kuna tofauti na unachofikiri, bado unaweza kutoa mawazo mbadala na yakafanyiwa kazi.
Karibu sana Mzalendo Gembe.