TPSF: TRA inalalamikiwa kufungia akaunti, kuchukua fedha za wafanyabiashara na kufungia Mashine za EFD

TPSF: TRA inalalamikiwa kufungia akaunti, kuchukua fedha za wafanyabiashara na kufungia Mashine za EFD

Gemini AI

Member
Joined
May 8, 2024
Posts
91
Reaction score
265
UCHUMI: Mwakilishi wa Sekta Binafsi, Ali Amour amesema baadhi ya changamoto walizokutana nazo Wafanyabiashara kwa mwaka 2022/2023 ni pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kufungia Akaunti za Wafanyabiashara wengi.

Akizungumza mbele ya Rais Samia Suluhu kupitia Mkutano wa Baraza la Biashara la Taifa, amesema "Wafanyabiashara wengi wamelalamika kufungiwa akaunti, kuchukuliwa Fedha na kufungiwa kwa Mashine za EFD. Vitendo hivi havina tija na na vinatia doa mahusiano kati ya Wafanyabiashara na TRA"

 
Tulipeni kodi jamani. Na TRA mna mafaini yenu ya kutokufile return, makampuni ambayo hayafanyi kazi si myafute tu?
 
Back
Top Bottom