TRA ASCUDA, kulikoni?

GeniusBrain

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2010
Posts
4,315
Reaction score
309
Ndugu wana bodi,

Najua humu ndani ya Jukwaa letu la JF lina wanachama na wapenzi ambao hupitia humu ndani mara kwa mara. Kwa maana hiyo basi , ujumbe unao wekwa humu husomwa na wengi.

Suala ni hivi, watu wa TRA ASCUDA huu ni uzembe wa hali ya juu. Kuna jamaa yangu aliagiza gari na amelipa ushuru kama ilivyokuwa inatatikana na gari tangia Jumatano wiki iliyopita ( 20.03.2013) ilitoka ila mpaka leo hii TRA hawajatoa kadi ya gari. Maelezo aliyoyapata ni kuwa, kuna mama mmoja tu kwenye system yao ya Ascuda ambae anatakiwa aingize data kwenye system , na tangia ijumaa mpaka leo hii hajafika kazini na hana mbadala wake. Kweli huu ni utendaji bora wa kazi kwa mamlaka kubwa kama TRA ambayo inategemewa na uchumi wa nchi ?. TRA tuache kufanya kazi kwa mazoea na kwa utaratibu wa kizamani, kama mtu hayupo wekeni mbadala wake. Mh. Kitilya hebu rekebisheni hili TRA mmekuwa na mfumo mbovu sana.
 
Kwa hiyo huyo mama akifa leo TRA ndo inakuwa imekufa?? Mi nahisi hayo ni majibu ya mzembe mmoja kwenye hicho kiseksheni
 
Kwa hiyo huyo mama akifa leo TRA ndo inakuwa imekufa?? Mi nahisi hayo ni majibu ya mzembe mmoja kwenye hicho kiseksheni

Mkuu ni mambo ya ajabu sana yanafanyika kwenye hiki kitengo, mtu tangia ijumaa hajafika kazini mpaka leo hii wao wala hawashtuki wanaona ni poa tu ili hali mtu aliisha timiza wajibu wake wakulipia kodi mpaka gari yake ikatoka, ametimiza wajibu wake. Na wao ukichelewa kulitoa gari wanakuchaji gharama za ziada kwa kuchelewa kulitoa, huu ni uonevu sana.
 
Mkuu hebu jiongeze kwa kuingia mfukoni na kunyoosha mkono. We huoni hapa jamaa wenye kuuza magari kwenye show rooms wanavyoingia na kutoka???

TRA hii ya CCM ni janga la kidunia, wanaona kama mlipa kodi ni mtu mwenye shida wakati inatakiwa kuwa vice versa
 
ASCUDA na siasa wapi na wapi!!!

Mpita Njia , TRA purely ni sehemu nyeti ya Serikali ambayo inakusanya mapato ya serikali kwa ajili yaku hudumia shughuli za maendeleo na za kawaida za serikali, huna njia yakuitoa ndani ya serikali . Na serikal ni sehemu ya siasa
 

Mkuu, sie ndio twatakiwa kuonyesha mfano wakupata haki zetu bila kutoa rushwa. Mtu ametimiza wajibu wake wakulipa kodi huna budi kumuheshimu na ww kutimiza wajibu wetu. Na kila siku wanatoa matangazo ya wananchi kulipa kodi bila kushurutishwa, wao kumbe msemo wao huo ni unafiki mtupu.
 
Tatizo siyo system ya Asycuda,tatizo wafanyakazi wa TRA wanakula deal na wenye ICDs akina
Kinana muua Tembo wetu,ili magari yalipe storage kubwa.
 

Mkuu hii TRA ilitakiwa kufanyiwa overhaul siku nyingi sana. Hiyo ASCUDA yenyewe hadi waliposhikiwa bakora ndio wakaanza kutumia. Wao walikuwa wanapenda ule mfumo wa zamani wa mafaili ndio walikuwa wanakula sana.

Sasa hivi kisingizio chao ni huyu mama yuko mmoja tu kwa hiyo njoo saa nane, ukienda saa nane wanakwambia njoo kesho asubuhi hadi wiki inapita. Ukiwatumia mawakala ambao wana mtandao nao kwa ile wanaita FAST TRACK siku mbili tu tayari una kadi ya gari tayari kwa kufuatilia insurance na plate number
 
Tatizo siyo system ya Asycuda,tatizo wafanyakazi wa TRA wanakula deal na wenye ICDs akina
Kinana muua Tembo wetu,ili magari yalipe storage kubwa.

Mkuu hili ni janga kwa kweli
 

Mkuu, umefika wakati tusikubali vitu vya namna hii, haki ya mtu isiuzwe kwa hali yoyote na TRA wangerekebisha mazongo zongo yao kama haya ushuru ungekusanywa sana.
 
Siku hizi koment zako ziko tofauti sana na zile za zamani... za siku hizi zinafana na jina lako

Mkuu, mie mtenda haki na napenda hai ukiona nasema tofauti ujue upande ule ninao usemea ndio wenye haki.
 
Mpita Njia , TRA purely ni sehemu nyeti ya Serikali ambayo inakusanya mapato ya serikali kwa ajili yaku hudumia shughuli za maendeleo na za kawaida za serikali, huna njia yakuitoa ndani ya serikali . Na serikal ni sehemu ya siasa
Alaaa, kumbe! Kwa maana hiyo TRA = SIASA? Sasa kama ni hivyo kwa nini mnashangazwa na hayo yaliyotokea?
 
Mkuu hili ni janga kwa kweli

ASSYCUDA ++ ni Janga la kitaifa.
Ukichukua masaa inayofanya kazi ni machache mno kuliko masaa inayokua inaumwa.

Cha kusikitisha zaidi ni kua hata kama yenyewe ndo itakua imezembea, bado mzigo unaangukia kwa mteja kulambwa storage za nguvu.

Nashawishika kuamini kua wenye hizi INLAND CONTAINER DEPOT wana mkono kwenye kushusha ufanisi wa hili janga ili watukamue storage
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…