Shark
JF-Expert Member
- Jan 25, 2010
- 29,775
- 29,746
Kwema Wakuu?
Naomba niende moja kwa moja kwenye mada. Tanzania ni nchi ambayo inaingiza au kuagiza bidhaa nyingi kutoka nje. Bidhaa hizi zinaweza kua za mahitaji au matumizi binafsi, bidhaa za biashara, bidhaa kwa ajili ya kutoa huduma, etc.
Ukiacha bidhaa hizi zinazoagizwa sasa, wapo pia wengine wangependa kuagiza lakin wanashindwa kwa kuogopa ushuru ulivyo mkubwa. Kwamba wanaweza kagiza kisha mizigo ikafika kwa wakati ambao mambo ya fedha yameyumba mizigo ikaishia kupigwa mnada bandarini ikawa hasara kwao.
Ushauri wangu ni kwa mamlaka ya mapato kuruhusu waagiza bidhaa KULIPA KWA AWAMU (INSTALLMENTS). Yaani mfano nimenunua gari ushuru ukaja labda 9Mil basi kuwe na maximum miezi 6 labda ya kulipa kwa awamu. Naweza nikawa natoa japo 1.5Mil kia mwezi kulipa TRA ili after 6months niwe nimemaliza deni la 9Mil.
Hii itawawezesha wengi kuagiza bidhaa hizi kutoka nje ya nchi wakijua kua mzigo utakapofika bandarini basi watakua wnaalipa kidogo kidogo mpaka kodi ikiisha. Mteja hatoruhusiwa kuchukua bidhaa zake mpaka atakapomaliza deni la kodi yake kwa hiyo miezi 6. Na ikitokea hapo kati mambo yakakaa vizuri basi amalizie tu deni lilobaki.
TRA inaweza kujenga "ma-godown" ya kuhifadhi hizo bidhaa (bonded warehouse) na ikawa inalipisha kodi ya kuhifdhi mizigo kwa gharama rafiki tu. Inaweza ikaonekana kama inachelewesha mapato kwenye mamlaka lakini kwenye uhasibu kuna kitu kinaitwa "acrrual", ambapo kwa muktadha huu ni kua mapato yatahesabiwa pale tu mzigo utakapoingia, na sio mpaka malipo yake yawe yamefanywa yote.
Hili likifanyika, litawashawishi wengi zaidi kuagiza bidhaa nje, walipa kodi wataongezeka na hata kwenye hizo bonded warehouse mapato pia yataongezeka. Ingawa Ki uchumi kuagiza bidhaa nje ni hasara zaidi kuliko kutumia bidhaa zako za ndani, lakini sababu ni swala ambalo haliepukiki basi serikali haina budi kuweka mazingira mazuri ya uagizaji huo.