TRA Customs automated system

TRA Customs automated system

Voice of Wisdom

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2011
Posts
537
Reaction score
240
wakati nipo chuo cha kodi(institute of tax administration) nilisoma "trade facilitation" na njia mojawapo ambayo idara ya forodha walikubaliana na WTO ni kutumia "automated data system as under Kyoto convection" lengo likiwa ni kurahisisha biashara ya kimataifa.
Huu mpango ni mzuri sana kwa sababu unarahisisha mawasiliana kati ya "customs" na "clearing agents" na mizigo kutoka kwa wakati(kwa nchi makini)
sasa leo vow sipo hapa kuelezea sana juu yake ila kuhoji ni kwa jinsi gani Tanzania ilikuwa imejiandaa kutumia "customs automated data system?"
kwa nini nimeuliza/nimekuwa na shaka kama tulijianda au la?
Hi ni kutokana na adha ambayo wakala wa forodha tunakutana nazo mara kwa mara juu ya "system" kuwa chini na kushindwa kufanya kazi za wateja wetu kwa wakati.
Nina mfano unaoishi 'kuanzia ijumaa ya wiki iliyopgita system ipo chini sana hakuna mawasiliano kati ya tra na wakala wa forodha wala benki zinazohusika kupokea hzo kodi za forodha.
Wale wanaofanya kazi "airport cargo section" au mliotuma/kutumiwa mizigo mtakuwa mmepata hii shida sio tra wala twiga bank wanaweza kufanya kazi pale airport kwa sababu system ipo down.
Mizigo inatakiwa kulipia kodi, unalipiaje wakati hakuna mawasiliano kati ya tra na twiga?
Au wengine wanahitaji kuandikiwa release order" wataandikiwaje wakati system ipo down?
Kinachokera na kinachonifanya nijiulize je tulikuwa tumejianda si system kuwa down ila ni muda iliyokuwa down, embu fikiria kuanzia ijumaa jioni hadi leo muda huu system ipo down, yaani ni kama hakuna syrtem administrator wa kutatua hili tatizo.
Swali langu "je ni kwa kiasi gani tanzania ilijiandaa katika hili?
 
Asante sana kwa kutujulisha hili mkuu. Mimi nilikuwa naongea na agent wangu siyo muda mrefu akaniambia hajafanya malipo TRA eti hakuna system tangu Ijumaa. Nilidhani ndo uongo wa maagent lkn sikuwa na taabu sana kwani hata meli imefika lakini eti haingia bandarini. Kweli hii nchi ni Mungu tu atakayetusaidia.
 
ni kweli meli inaweza ikawa imefika na ikashndwa kuingia bandarini kwa kukosekana nafasi ya kupakulia mzigo wake.
 
Hii mifumo ya kitechnologia (Automation) kwenye idara za serikali imekata maulaji ya waajiriwa wengi.Ni lazima waikosoe na walie nayo.Kila kitu kikiwa kwa system mwanzoni kinausumbufu ila mtazoea tuu baadae mtakuwa kama nchi nyingine.Mannually serikali inaibiwa sana na usumbufu kwa wateja pia.
 
mkuu pengine hujapata hoja yangu, hoja yangu si kupunguza watu ila hoja yangu ni jinsi gani serikali ilijiandaa
1. Kimiundombinu
2. Kuwa na "skilled and expirienced expert" wa automate data system katika customs?
Haiwezekani kama walikuwa wamejianda vya kutosha kukawa na haya matatizo ya system kuwa down kwa zaidi ya siku tatu na mara nyingine hata wiki! Na hii inaadhiri biashara ukizingatia vitu vingi vinakuwa imported, na kibaya zaidi port wanapokuchaji storage charge hawazingati swala la system kuwa down ambayo ndiyo iliyopelekea mzigo wako kuchelewa kutoka
 
Nilimaanisha hizo kasoro ni za kufanyiwa kazi haraka, Na sio kutake adavantage kuwa kusiwepo na hizo system.Pia sikumaanisha technolojia inapunguza watu nilimaanisha Technolojia inadhibiti wizi.Mfano zamani mabenki yalikuwa yanafanya shughuli zake mannualy, wizi ulikuwa mkubwa.TRA walmetuletea machine zao Mapato ya nchi yakavuka malengo.Marekebisho na maboresho ya mifumu hii ndio cha msingi zaidi
 
Back
Top Bottom