mwanamichakato
JF-Expert Member
- Mar 20, 2015
- 1,188
- 1,090
Tanzania ni lango kuu la kupokea,kisafirisha mizigo inayoingia na kutoka ktk nchi takribani 7.Uwekezaji mkubwa ktk bandari zetu na miundombinu ya Reli,barabara,Mabomba na anga ni ushahidi tosha wa umuhimu wa taifa letu kijiografia.
Kila mwaka tunapokea mamilioni ya shehena za mizigo mbali mbali (Containerised,Bulk,Liquidfied,Vehicles,Equipments,etc) inayopita (transit imports,Transit exports) kwenda na kutoka Zambia,Malawi,DRC,Rwanda,Burundi,Zimbabwe,Angola,Uganda na South Sudan.
Ukiacha vituo vya customs vichache asilimia kubwa ya wasafirishaji hubeba dhamana kubwa (Take high risks) kuegesha malori yenye shehena ya mizigo,magari ktk vituo vya mafuta (Kimsingi wenye vituo wamewekeza kwa kijenga yards,Ulinzi na Vyoo/Mabafu)au parking yards binafsi njiani mipaka na mipakani licha ya mahitaji ya sehemu bado kuwa makubwa kuliko uwepo wake.
Sasa katazo lililotolewa linalokataza wasafirishaji kupaki magari yenye mizigo au magari yanayosafirishwa linakinzana na mapana ya uhalisia wa uwepo wa sehemu maalumu,changamoto ya usalama na athali za kisekta.Uwekezaji mkubwa ulipaswa kufanyika rasmi kwa kuzihusisha halmashauri zote zenye kuguswa na sekta ya usafirishaji kimataifa au ktk njia kuu kwenda ktk mataifa jirani.
Kama ambavyo Zambia,Zimbabwe na Africa kusini wamefanya yatengwe maeneo,Parking zijengwe zikiwa na huduma muhimu za kibinadamu,burudani na usalama.Hili lingechochea maendeleo ktk maeneo husika na kukuza mapato na uchumi.
Suala la ukwepaji kodi kwa baadhi ya wafanyabiashara kwa kuhusisha baadhi ya wafanyakazi wa TRA na wauzaji wa ving’amuzi lipo na linaweza kudhibitiwa kwa kuweka mikakati sawia ikowamo kupunguza kodi ambazo ni kikwazo ktk ufanyaji biashara,Hatua kali baada ya Comprehensive Forenscic lifestyle audits kwa watumishi wa mamlaka..Mwisho Mapapa wa uchepushaji mizigo (Wanajulikana) kushitakiwa,kufungiwa kufanya biashara Tanzania,Kufutiwa leseni zao za kibiashara..
Mwisho,Usalama wa mizigo ya Wateja wanaotumia bandari zetu ni suala muhimu kwa uchumi wa Taifa letu sasa na tuendako..Tusikurupuke ktk maamuzi yanayoweza kuleta usumbufu,madhara na utaabishaji.