TRA: GARI ALILOKUJA NALO MTANZANIA NCHINI TARATIBU NA GHARAMA ZA USAJILI WAKE NCHINI NI ZIPI?

Baba, uagize au ujenalo au upewe zawadi Taratibu ni zile zile. Fanya inspection huko huko, Tafuta carrier alibebe hadi bongo. Wakabidhi Clearing Agents Documents wafanyekazi. Lipia Dues na Duties zote. Hata kama gari umepewa bure ujue lazima watatumia Current value ya market kwa wakati huo.

Mambo ni mengi. Ila hakuna step ya kuskip hata moja
 
otherwise aje alipe ushuru wa kulitembelea nchini afu arudi nalo alikolitoa la sivyo kodi kodi kodi kodi
 
Yaaah anaweza kufanya Tempolary import na baadae anaweza rudi na gari lake
otherwise aje alipe ushuru wa kulitembelea nchini afu arudi nalo alikolitoa la sivyo kodi kodi kodi kodi
 
Temporary import ina cost kias gan? Maana December inatuhusu kurudi home tulio kimbia nchi kwa ukata wa pesa
 
Hii nchi kizunguzungu kingi hasa Tra na uhamiaji jumlisha polisi ni kichefuchefu
 
Mwenye kujua taratibu za temporary import atujuze hapa tafadhali.
 
Mkuu mfano nina gari yangu ambayo nimekuwa nikiitumia South Africa na nikataka niifute usajili sauzi nije nayo Tanzania kwa kuiendesha na niisajili. Gharama nitakazolipa TRA ni sawa na za mtu anayeagiza gari kama hiyo toka nchi kama Japan?
 
Hakuna tofauti sana. Hata ukiagiza gari kutoka nchi za ulaya na kutoka japani huwa kuna utofauti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…