TRA ibadilishwe kuwa Jeshi Usu

TRA ibadilishwe kuwa Jeshi Usu

and 300

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2012
Posts
26,398
Reaction score
36,406
1. Hii Migomo inaonyesha wafanyabiashara Kariakoo na kwingineko wanaleta mchezo kwenye kulipa kodi.

2. Inafaa Sasa TRA libadilishwe kuwa Jeshi Usu kama taasisi za Maliasili, Misitu.

3. Wafanyakazi wote TRA waende kozi ya awali ya ukakamavu, ujasiri na Nidhamu.

4. Kamishna Mkuu TRA ateuliwe toka vikosi vya Ulinzi na Usalama JW, KMKM au JKU.

**Ikibidi mtalipa Kodi Kwa shuruti.
 
1. Hii Migomo inaonyesha wafanyabiashara Kariakoo na kwingineko wanaleta mchezo kwenye kulipa kodi.

2. Inafaa Sasa TRA libadilishwe kuwa Jeshi Usu kama taasisi za Maliasili, Misitu.

3. Wafanyakazi wote TRA waende kozi ya awali ya ukakamavu.

4. Kamishna Mkuu TRA ateuliwe toka vikosi vya Ulinzi na Usalama JW, KMKM au JKU.
hamna taasisi duniani imewahi kubadili vyombo vyake vya kukusanya kodi kuwa jeshi. Unajua msingi wa kuanzishwa kwa jeshi?
 
Wafanyabiashara siku zote hawataki kulipa Kodi kuna wakati wanajifanya wanyonge wanaojua kuongea uongo na kusikilizwa lakini lila Mtanzania ni shahidi jinsi wanavyo toa risiti na kuandika uongo kukwepa uhalisia.
 
Duuh haya mambo yangekuwa yanazungumzwa wakati wa Magufuli ungesikia Dikteta uchwara.

Ila kwakua ni awamu yao basi ni sawa tu.

Hapa wanatuzuga wapo serious kwakua tunakaribia uchaguzi tukishawarejesha waendelee kutupiga.
 
Utake usitake CCM ndo mshindi
 
Tukitaka TRA wafanye kazi kwa ufanisi kama IRS (ya marekani) LAZIMA tuondoe porojo na ubabaishaji wa kisiasa kwenye ukusanyaji wa kodi. Hiyo ndiyo solution pekee.
 
Shida sio Kodi kukusanywa bali ni matumizi ya hizo Kodi. Ingalikuwa mtu akidokoa hata buku kwenye mfumo anasomewa hukumu kibaharia Wala usingesikia malalamiko ya kijinga juu ya ukusanyaji Kodi. WATU wangelipa maana wanajua Kodi inaleta unafuu wa maisha Kwa kiwango gani.

TUNAHIMIZANA KULIPA KODI ILI KUNDI FLANI LA WATU WAFANYE MATANUZI YA ANASA NA KUDHIHAKI RAIA KANA KWAMBA HAWANA AKILI NA HILO KUNDI KUJIONA BORA NA DARAJA LA JUU KULIKO WATANZANIA WENGINE? HALIJAKAA SAWA KABISA...WATANZANIA SIO WAJINGA, SERIKALI IWAJIBIKE HASWA HATUNA SABABU YA KUFADHILI MAMBO YA KIJINGA WAKATI MAMBO YA MSINGI YALIOTAKIWA YAFADHILIWE NA KODI ZETU YANAKWEPWA. TUCHANGE KODI ILI WAPAMBE WAPELEKWE KOREA KUVAA MAGUO NA KUFANYA COMEDY MITANDAONI WAKATI KINA MAMA WAJAWAZITO WANAKUFA KILA KUKICHA KWA KUKOSA HUDUMA STAHIKI MAHOSPITALINI?
 
1. Hii Migomo inaonyesha wafanyabiashara Kariakoo na kwingineko wanaleta mchezo kwenye kulipa kodi.

2. Inafaa Sasa TRA libadilishwe kuwa Jeshi Usu kama taasisi za Maliasili, Misitu.

3. Wafanyakazi wote TRA waende kozi ya awali ya ukakamavu, ujasiri na Nidhamu.

4. Kamishna Mkuu TRA ateuliwe toka vikosi vya Ulinzi na Usalama JW, KMKM au JKU.

**Ikibidi mtalipa Kodi Kwa shuruti.
Salute!
 
Back
Top Bottom