Juzi kati nilikuwa katika mishe zangu za harakati za kupambania mkate wa kila siku ambayo ilihusisha uuzaji wa nyumba. Biashara ikafanyika vizuri na mwisho wa siku dalali akaondoka na Shilingi 10.
Tangu siku hiyo nimekaa nikiwaza ni kiasi gani cha mapato Serikali inapoteza kama kodi kutoka katika sekta isiyo rasmi. Licha ya nchi yetu kuwa na watu zaidi ya milioni 60 ila walipa kodi hawazidi milioni 2 na wakati huohuo TRA imesajili walipa kodi wasiozidi milioni 5.
Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Chande akihutubia Bunge tarehe 6/9/2023 alidai sekta isiyo rasmi inakadiriwa kuajiri watu karibu milioni 27.7, Swali je, ni wangapi wanalipa kodi halali? na Serikali imechukua hatua zipi ili kuwawezesha watu hao kulipa kodi?
Sheria za kodi za Tanzania zina mtambua mtu mwenye kipato cha kuanzia Sh 270,000/= kulipa kodi ila wanaolipa kodi kwa sasa ni wale walio katika mfumo rasmi wa ajira, walio nje ya mfumo rasmi wa ajira hawalipi kodi hata kama kipato chao kinazidi kiwango cha laki mbili na sabini.
Sekta ya Udalali kwa miaka ya hivi karibuni imekua sana na imeingiliana na sekta kama kilimo, real estate, utalii, biashara nk ila mchango wake katika kuongeza mapato ya nchi kupitia kodi naweza kusema ni sawa na sifuri kabisa licha ya kwamba wanaingizi pesa nyingi.
Madalali wa nyumba, viwanja, magari wamekuea wakijipatia kipato kikubwa bila ya kulipa kodi kwa Serikali, kuna wakati wanachukua mpaka Asilimia 10 ya malipo ya walichodalalia.
Fikiria dalali anayeuza kiwanja/nyumba Kariakoo anaondoka na kiasi gani cha mapato? Kuna case madalali wanaondoka mpaka na Sh Milioni 50+ kwa kuuza jengo moja na wala hawalipi kodi sababu wapo kwenye sekta isiyo rasmi.
Kuna madalali wa mazao ambao wanafaidika kuliko Wakulima, ukirudi sekta ya uvuvi nayo wavuvi na walio kwenye mnyororo wa thamani wa uvuvi wengi wao hawalipi kodi, hivyo Serikali kukosa mapato.
Wito wangu kwa Serikali na hasa TRA watafute njia za kuingiza sekta isiyo rasmi katika ulipaji wa kodi maana uko ndipo hela nyingi ilipo.
Nchi kubwa kama hii yenye watu zaidi ya milioni 60 haiwezi kuendelea kwa kuwa na walipa kodi wasiozidi milioni 2 tena ambao hawalipi kodi kihalali, kila mtu anapaswa kuchangia maendeleo ya nchi yetu na maendeleo haya yanaletwa kwa kulipa kodi.
TRA wanatakiwa kuja na mbinu rafiki na madhubuti kuhakikisha watu wote wanaostahili kulipa kodi basi wanalipa kodi stahiki, kama TRA inaweza kukusanya kodi hadi kwenye maduka ya rejareja (kwa mangi) yalipo mitaani basi pia inaweza kukusanya kodi kwa madalali waliopo mitaani.
Mfano mosi, kuhakikisha kila mwenye nyumba / jengo / kiwanda / gari au mali yoyote inayouzwa kuwasilisha makato aliyomkata dalali la sivo basi yeye mnunuzi ndio atawajibika kulipa makato hayo.
Pili, kufatilia na kujiridhisha na miamala ya fedha ya kila mtu kama ni halali na imelipiwa kodi stahiki kuhakikisha kila kipato kinachoonekana katika miamala ya kibenki, simu nk imelipa kodi stahiki, maana leo hii Mtanzania anaweza kufanya miamala ya kibenki au simu bila kuulizwa chanzo cha kipato chake na kama kimelipiwa kodi.
TRA ikitaka kuongeza wigo wa kukusanya kodi basi sekta isiyo rasmi ndio mahali sahihi pa kuanzia kukusanya kodi ila kwa njia rafiki