TRA inatarajia kukusanya Sh trilioni 3.49 kwa Desemba, 2024

TRA inatarajia kukusanya Sh trilioni 3.49 kwa Desemba, 2024

Dalton elijah

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
373
Reaction score
829
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) inatarajia kukusanya Sh trilioni 3.49 kwa Desemba, 2024 kiasi ambacho hakijawahi kukusanywa tangu kuanzishwa kwa mamlaka hiyo.

Kadhalika, imepanga kuanzia Januari hadi Juni, 2025 kukusanya Sh trilioni 15.27 ili kuhakikisha wanafikia lengo la kukusanya Sh trilioni 31.05 kwa mwaka wa fedha 2024/2025.

tra2.jpg

Mkurugenzi wa Fedha wa TRA, Dinah Edward amesema hayo walipokutana na wafanyakazi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwa ajili ya kuwashukuru.

Amesema ushirikiano kati ya BoT na TRA umewezesha kukusanya Sh trilioni 12.94 hadi kufikia Novemba mwaka
huu sawa na asilimia 100 ya mapato ghafi na asilimia 47 ya makusanyo kwa mwaka mzima.

Ameeleza usimamizi unaofanywa na BoT kwa benki na maboresho ya mifumo ya uhamishaji wa fedha ina mchango mkubwa katika kupanua wigo wa walipakodi na kurahisisha ulipaji wa kodi.

“Usimamizi wa mapato unaratibiwa na TRA lakini ninyi mmekuwa chachu ya kuchangia ufanisi wetu na tunaamini tukiendelea kushirikiana tutafika hatua ya juu zaidi kwa manufaaa ya nchi,”amesema Edward.


tra3.jpg



Ameongeza kuwa makadirio ya makusanyo waliyojiwekea kwa Desemba hayajawahi kukusanywa tangu kuanzishwa
kwa mamlaka hiyo.

Kwa upande wake, Gavana wa BoT, Emmanuel Tutuba amesema wanatambua umuhimu wa kulipa kodi, hivyo wao ni mawakala wa kukusanya kodi kutoka kwa wadau na kuwasilisha kupitia mifumo.

Amesema wao wanalipa kodi kutokana na makadirio na maeneo yao na kwamba wana wajibu wa kusimamia sekta ya fedha kuwezesha mamlaka hiyo kuongeza ufanisi na tija katika ukusanyaji wa mapato.
”Tumejipanga vizuri kuwezesha ukusanyaji kodi katika kipindi hiki cha sikukuu kwani mifumo yetu iko vizuri kuruhusu miamala ipite na tutafanya kazi saa 24 kuhakikisha mifumo imara na benki zote zitaongeza muda wa kufanya malipo kuirahisisha mtu anayetaka kulipa,’’ ameeleza.


tra4.jpg


Amesema kila mmoja anapaswa kutumia mifumo ya fedha iliyopo ikiwemo Mfumo Jumuishi wa Kieletroniki (TIPS), Mfumo wa Malipo Makubwa na ya Haraka (TISS) na Mfumo wa Malipo ya hundi au malipo madogo ya kielektroniki
(TACH).

Amesema kupitia mifumo hiyo, imepunguza gharama ya uhawilishaji fedha na kuwezesha Watanzania kufanya malipo kutoka benki na kupitia simu ya mkononi.

“Niwatoe wasiwasi kwamba akaunti zote za fedha za serikali, za benki na kwenye simu za mikononi ziko salama licha ya majaribio ya mara kwa mara ya udukuzi, hakuna hatari iliyofanikiwa,” amefafanua.
 
Hii ya kila mwaka ni makusanyo ambayo hayajawahi kukusanywa toka kuanzishwa kwa mamlaka, ni stori ya kila mwaka, mwaka juzi ilikua hivyo, mwaka jana ilikua hivyo, waka kesho itakua hivyo, mwaka keshokutwa itakua hivyo na miaka yote, haina maana yoyote kwa sababu ni kitu kinachotarajiwa.

Stori zile zile kila mwaka.
 
Kujitathmini kwa TRA: Kwanini Serikali isiunde Chombo cha Kuisimamia?

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ina jukumu muhimu katika ukusanyaji wa mapato ya serikali. Hata hivyo, kuna maswali mengi yanayojitokeza kuhusiana na ufanisi wake na uwazi katika shughuli zake.

Kwanini serikali isiunde chombo cha kuisimamia na kuisemea TRA katika kukusanya na kutangaza mapato yake?

Kwanza, ni muhimu kuelewa kwamba TRA ni chombo cha serikali kinachohusika na ukusanyaji wa mapato kupitia kodi. Hivyo, inafanya kazi kwa kujitegemea bila usimamizi wa moja kwa moja kutoka kwa serikali.

Hii inapotajwa, kuna hatari ya ukosefu wa uwazi katika taarifa zinazotolewa kuhusu makusanyo. Ikiwa TRA inakusanya na kutangaza mapato yake bila chombo kingine cha kuangalia, kuna uwezekano wa kushindwa kutoa taarifa sahihi kuhusu makusanyo hayo.

Hii inaweza kuleta shaka kuhusu uhalali wa ripoti hizo na kuathiri imani ya umma kwa TRA.

Pili, ni muhimu kuzingatia kuwa TRA ina jukumu la kukusanya mapato, lakini pia ina jukumu la kuunda sera za kodi. Hii inamaanisha kuwa inaweza kuwa na maslahi binafsi katika kuonyesha makusanyo kuwa makubwa ili kuhalalisha sera zake. Ikiwa hakuna chombo huru cha kuangalia, ni vigumu kwa umma au wadau wengine kujua ukweli kuhusu hali ya makusanyo.

Hali hii inaweza kupelekea kutokuelewana na ukosefu wa uwajibikaji.

Tatu, chombo huru cha kuisimamia TRA kingeweza kusaidia katika kuboresha ufanisi wa ukusanyaji wa kodi. Kwa mfano, chombo kama hicho kingeweza kufanya tathmini ya mifumo ya ukusanyaji wa kodi na kutambua maeneo yanayohitaji kuboreshwa.

Hii ingesaidia TRA kuwa na mikakati bora ya kukusanya mapato zaidi kwa njia inayofaa na yenye uwazi.

Pia, kutokuwepo kwa chombo cha kuangalia kunaweza kuathiri uwezo wa serikali wa kuweza kupokea taarifa sahihi kuhusu hali ya uchumi. Serikali inahitaji taarifa sahihi ili kufanya maamuzi mazuri katika mipango ya maendeleo.

Ikiwa TRA inakusanya na kutangaza makusanyo yake yenyewe, inaweza kuwa vigumu kwa serikali kupata picha kamili ya hali ya uchumi wa nchi. Hii inaweza kuathiri mipango ya maendeleo na hata uwekezaji wa kigeni.

Kwa upande mwingine, ni muhimu kuzingatia kuwa serikali ina wajibu wa kuwapa wananchi taarifa sahihi kuhusu matumizi ya mapato yanayokusanywa na TRA.

Ikiwa hakuna chombo huru cha kuangalia, ni vigumu kwa wananchi kujua jinsi mapato yanavyotumiwa na kama yanatumika kwa malengo yaliyokusudiwa. Hii inaweza kupelekea kukosekana kwa uwazi na uaminifu katika utawala wa fedha za umma.

Kwa kumalizia, kuna haja ya serikali kuunda chombo cha kuisimamia na kuisemea TRA katika ukusanyaji na utangazaji wa mapato.

Kutokuwepo kwa chombo kama hicho kunaweza kupelekea ukosefu wa uwazi, uaminifu, na ufanisi katika shughuli za TRA.

Hii inamaanisha kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kuweka mifumo ambayo itasaidia kuboresha ukusanyaji wa kodi na kuhakikisha kuwa taarifa sahihi zinapatikana kwa umma na serikali.

Ni lazima serikali iangalie kwa makini jinsi ya kuimarisha uwajibikaji katika TRA ili kuhakikisha kuwa inatimiza majukumu yake kwa ufanisi na kwa faida ya wananchi wote.
 
Hayo makusanyo yanahusisha mazaga yote yakiwemo matozo ya kwenye;
  • Umeme
  • Mafuta
  • Mawasiliano
  • VAT
  • PAYE
  • Import
  • Customs
  • Withholding
  • Biashara
  • Halmashauri, miji, etc
  • Kodi za ardhi
  • Gawiwo
  • Mrabaha(Sijui Mirahaba)
-
-
-
????

Au zinahusika na eneo maalum?
 
Back
Top Bottom