TRA Jifunzeni hapa aina 3 za kodi muhimu China

TRA Jifunzeni hapa aina 3 za kodi muhimu China

mirindimo

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2009
Posts
901
Reaction score
1,742
1. VAT
Kama robo mwaka turn over yako ni zaidi ya RMB 300,000 (TZS 100mil+) tax rate ni 1% otherwise no VAT

2. PROFIT TAX
Kama profit yako ni zaidi ya RMB 3mil (TZS 1bil +) tax rate ni 25% chini ya hapo utalipa tax rate ya 5%

3. PERSONAL INCOME TAX
Kama mshahara wako kwa mwezi ni RMB 10,000 (TZS 3mil+) tax rate ni RMB 290

Kwanini TRA wasijifunze kuweka aina za kodi rafiki kama hizi ili watu wengi wavutike na kushawishika kulipa kodi?
Nchi yetu ni maskini lakini mzigo wa kodi kubwa kwa mwananchi haimaanishi kufanya nchi iendelee, bali tukiwa na kodi rafiki tukaongeza walipa kodi watu wengi watajitokeza kulipa kodi na nchi itasonga kwa kasi na hapatakua na ukwepaji wa kodi kama ilivyo sasa.
 
Screenshot_2024-07-01-18-50-55-467_com.openai.chatgpt.jpg

Tuwe tunaacha kutoa habari za uongo
 
Bila source za kueleweka ni sawa na bure
 
Kwanini TRA wasijifunze kuweka aina za kodi rafiki kama hizi ili watu wengi wavutike na kushawishika kulipa kodi ?
Hawawezi kwa sababu wakubwa wanatakiwa kulipa madeni waliyokopa huko nje ili wanunue VXR zao na za wake zao
 
Hata kodi ya mshahara (PAYE) haieleweki inakokotolewaje. Wanasema ni 'single digit' lakini kiukweli sivyo!
 
Sijatoa habari za uongo achana na ChatGPT nenda China mimi nilienda Physically acha kuamini maroboti haya... ndio maana mnalawitiwa achaneni na haya maroboti
Weka documents zinazosapoti hoja yako
 
Mkuu waweke tax za hivyo alafu wewe ndio utawanunulia ma land cruiser Prado LC300, au wewe ndio utakuwa unawalipia kina Steve Nyerere kwenye maziara ya Korea huko sijui na wapi?
Aisee! Na hela za kuwanunua wapinzani zitapatikana kweli kama kodi itakuwa rafiki! Hizi teua tengua za kuwapangia watu kazi nyingine, na zenyewe ndiyo zisifanyike tena!!
 
Hata kodi ya mshahara (PAYE) haieleweki inakokotolewaje. Wanasema ni 'single digit' lakini kiukweli sivyo!
paye inaeleweka mbona, kwenye basic unaondoa pension then the rest ni taxavle in this rate

270,000-520,000 tax ni 8%
520,000-760,000 tax ni 20%
760,000-1,000,000 tax ni 25%
1,000,000 tax ni 30%
 
Back
Top Bottom